Wakazi wa Jiji la Mbeya leo wamejikuta wakiwa katika mazingira magumu baada ya mgomo wa mabasi madogo wa kutopakia abiria kutoka stendi kuu jijini humo,wakitaka wabadilishiwe ruti au kuongezewa nauli kwa sababu ya ruti hiyo inawapa mzungunguko mkubwa sana kulinganisha na nauli wanayoichaji kwa abiria hao.hali hiyo imepelekea abiria mbali mbali wa jiji hilo kupanga kwenye pikup na kulipa nauli ile ile wanayolipa kwenye daladala kama ionekanavyo katika picha mbali mbali zilizopigwa na Mpiga picha wa Globu ya Jamii,jijini Mbeya, Fadhil Atick.
Abiria jijini Mbeya wakiwa ndani ya lori kuendelea na safari zao.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa jijini Mbeya mchana wa leo.
Wengine walikuwa wakigombea kwenye Bajaj.
Hali ilikuwa tete.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...