Wananchi wa Kijiji cha Kitwai A wakiwa wamenyoosha mikono juu,kwenye mkutano wa hadhara,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akimuunga mkono jambo Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka,katika suala zima la Utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Pichani
mbele ye bango kulia ni jengo la Mama na Mtoto la kituo cha Afya
Orkesument,Wilayani Simanjiro,ambalo pia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
alikagua na kujionea ujenzi wake.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimsikiliza Dkt.Juma Nahonyo wakati wa
ukaguzi wa jengo litakalokuwa bohari ya Dawa katika kituo cha Afya cha
Orkesument,kulia ni Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka.

Kinana
ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,wako moani Manyara kwa ziara ya siku saba ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa
kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za
mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.

Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua gari la mradi wa
Kukodisha la Kikunndi cha Vicoba Mkombozi chenye wanachama wapatao
30,mjini Orkesument,Wilayani Simanjiro mkoani Manayara.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa Kikundi cha
Mazingira kilichopo mjini Orkesument,Wilayani Simanjiro mkoani
Manayara.Kikundi hicho kitatumika kuwaelimisha wananchi wa mji huo katika
masuala ya usafi na kulinda mazingira,kuwaelimisha wananchi kuhusiana
na mambo ya maambukizi ya UKIMWI,masuala ya Rushwa na mengineyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh.Ole Sendeka wakati akiangalia josho la ng'ombe la Orkirung'rung ambapo kuna mradi wa ufugaji wa ng'ombe chotara,ufugaji wenye tija na unaosaidia kuongeza thamani mifugo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh.Ole Sendeka wakati akiangalia josho la ng'ombe la Orkirung'rung ambapo kuna mradi wa ufugaji wa ng'ombe chotara,ufugaji wenye tija na unaosaidia kuongeza thamani mifugo.
Baadhi ya Wanahabari pichani kati shoto ni Mwinshehe kutoka gazeti la Jambo Leo na Mary kutoka Gazeti la Nipashe wakiwa sambamba na wafuasi wa chama cha CCM,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kitwai A,wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwenye zaiara ya Katibu Mkuu wa CCM.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...