Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo matano, sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kjinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma. kushoto kwake ni Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu –Usiri na Mkurugenzi wa Mfuko wa vyombo vya habari, Ernest Sungura.(Picha zote na Zainul Mzige).
Na Damas Makangale
WAANDISHI WA HABARI nchini wamehimizwa kushirikiana kwa karibu na Mfuko wa Vyombo vya Habari (TMF) ili kuacha kutegemea zaidi matangazo kwa sababu kuna weka taaluma yao rehani.
Akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari jinsi ya kuripoti mambo ya sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kijinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya na watayarishaji wa vipindi vya luninga, Waziri wa kazi na Ajira, Mhe, Gaudensia Kabaka amesema kwamba vyombo vya habari lazima vishirikiane na mfuko huo ili kuwa huru wakati wa kuripoti.
“kuendelea kutengemea matangazo kutoka kwenye makampuni mbalimbali ili kujiendesha kuna wafanya kutokuwa huru katika uandishi wetu na tasnia ya habari kwa ujumla,” amesema Kabaka
Amesema mradi huo wa mafunzo ya bure kwa waandishi ni muhimu kwa taifa kwa sababu tatizo kubwa la ajira hasa kwa vijana na wanawake linachangia kwa kiasi kikubwa vijana wengi kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Baadhi ya wadau na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...