Mchora vibonzo, Nathan Mpangala akiwa mbele ya gofu la Makutano Palace lililo Kilwa Kisiwani, Lindi hivi karibuni. Hakika Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo!
 Mchora vibonzo, Nathan Mpangala akiwa makaburi ya Familia ya Sultani wa Kilwa, Al Hassan Bin Suleiman, Kilwa Kisiwani, Lindi hivi karibuni. Makaburi haya yanayodaiwa ya karne ya 16 yana alama ambazo ni rahisi kugundua lipi la mwanaume na lipi la mwanamke.
Mchora katuni, Nathan Mpangala (mwenye sanigogozi) akisikiliza simulizi toka kwa wenyeji wa Kitongoji cha Masakasa Mpala, Kilwa Masoko, Lindi hivi karibuni. Mzee Hamis Sumri (aliyetinga kitu cha Arsenal) anasema, sifa moja ya kitongoji chao ni hii; kiliwatoa Salum Chanza, Ali Juma, Idd Hamis na Mzee Juma kwenda kushiriki vita ya pili ya dunia kati ya Mjerumani na Mwingereza na walirudi salama salimini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2014

    SASA MBONA HATUFUNDISHI HISTORIA HII? TUTAJUAAJE? KAMA NI YA KARNE YA 16 BASI KULIKUWA NA CIVILIZED SOCIETY HAPO. SASA SIYE WATANZANIA TUPOTUPOJE??? YANI HATUJIJUI TUMETOKA WAPI N.K. KWELI TUNAWEZA KUENDELEA KIUCHUMI NA KISIASA KWA MTINDO HUU???

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2014

    mijitu mingine bhana! Ovyooo... Kwanza ufundishwe we na nani. Halafu kama umeweza kuingia humu hujui ku-google weye? acha ujuaji mmatumbi. Kama hujui ulikotoka na unataka utafuniwe hadi ulishwe kalagabaho.mijitu kama nyie mnachefua kujifanya kukosoa kila kitu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2014

    Anony No. 2 una chuki binafsi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...