Home
Unlabelled
kutoka maktaba: ikarus kumbakumba we miss you... post back by popular demand
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Acha tu! Sijui kwa nini tunaenda mbele hatua moja na kurudi hatua kumi nyuma!
ReplyDelete"Soon I will be back never mind"
ReplyDeleteKumbe uda kulikuwa na madereva wazungu, au jamaa ni mshihiri au baniani?
ReplyDeleteOhh Michuzi, unanikumbusha mbali sana wakati nchi yetu ilikuwa bado na mshikamano wa kweli na upendo!! Ufisadi ulikuwa bado haujakithiri, ndio maana hata kiongozi wa wakati huo anaonekana kama "Mtakatifu"!!
ReplyDeleteNaomba uwe unaposti picha nyingi za nyuma ili japo tujitafakari na turudishe ule utu na ubinadamu na ujasiriamali tuliokuwa nao wakati ule, maana licha ya hali ya kiuchumi kuwa tete, wananchi walijitahidi kuziba pengo kwa kutengeneza nguo (Mwanza karibu na mwaloni), sabuni, viatu na kandambili, mafuta ya kujipaka (tuliweza kuuza nje ya nchi kama Zambia na Malawi). Haya yote yalifanyika licha ya wakati mwingine mkono wa dola kutumia nguvu za ziada bila ya ruhusa kutoka juu (uhujumu uchumi n.k.)
Tusiporudia ujasiri wa wakati ule nchi inaondoka mbele ya macho yetu!!
Ewe Muumba ibariki Tanzania bara na visiwani!!
Zamani tulikuwa watu wastaarabu tulikuwa tunapanga mstari kuingia kwenye ekarusi siku hizi bho utafikiri mang'ombe. Hate it
ReplyDeleteyarudishwe tena jamani yalikuwa mkombozi tena haya hayahitaji kuwa na viti vingi.watu wanasimama na wanaenea wengi. mradi tu yatengewe njia kama wanavyosema public transport itapewa kipao mbele. wanafikiria mambo makuuubwa eti mabasi yaendayo kasi wakati ni kiasi tu cha kurudisha kitu kilicholwisha tumika na kikaonekana kufanya kazi vizuri ila tu usimamizi ulizorota. ekarusi namba wani amini usiamini yakiingia matatau barabarani yatakuwa yamechukua nafasi ya daladala 6. vurugu na foleni zitapungua.
ReplyDeleteNadhani huu Mpango wa Mabasi yaendayo Kasi Dart Jijini Darisalam wangerudusha tu mabasi haya yaliyokuwa ya UDA aina ya Ikarus tatizo la Usafiri lingekwisha!
ReplyDeletePia tiketi ya msimu yaani unakata tiketi ya basi la UDA ya mwezi mzima in-advance na unatumia kwa route zote za mabasi jijini DSM bila haja ya kulipia reja reja kila upandapo mabasi.
ReplyDeleteHaikuwa tofauti na jinsi usafiri wa 'ulaya-ulaya' wa umma ulivyo sasa yaani tiketi za msimu za wakubwa na watoto(pamoja na wanafunzi), taimu tebo (time schedule) ya mabasi inajulikana kila baaada ya dakika ngapi basi litawasili katika kituo husika n.k
Wazazi wanakununulua tiketi ya msimu inakuwa hakuna tena haja ya kuomba nauli kila asubuhi kuwahi shule.
Kama mdau hapo juu alivyosema tumerudi hatua kumi mara mbili nyumba ktk masuala ya usafiri wa umma wa mijini.
Mdau
Christos Papachristou
Diaspora
Hiyo picha ya Ikarus haikupigwa Bongo , na huyo dereva ni M-Hungary
ReplyDeleteEti tulikua tunapanga foleni wenyewe? Alikuwepo afande wa pale msimbazi aliyepanda cheo kwa kusimamia foleni, jina limenitoka kidogo ila alikuwa maarufu kwa mikogo ya aina yake. Pia walikuwepo Wabulgaria wenye pistol vibindoni wakilinda foleni. Mdau kumbuka vizuri!
ReplyDeleteAlikuwa anaitwa mkama sharp.
DeleteHaya mabasi bado yapo duniani na hata yalipotoka. Huku Marekani kwenye majimbo ya NewYork na miji mingine mikubwa where public transportation is the backbone for the means of going and come back from work.
ReplyDeleteIs not true?
Taifa hili linahujumiwa na wale tulio waamini kuwapa madaraka watuongoze.
ReplyDeleteUsafiri wa Dar hauhitaji bara bara maalumu.Tunahitaji nidhamu tu na usimamizi madhubuti.
Tujitathimini tuijenge nchi yetu.Kizazi kijacho kitatulaumu sana kwa kutoitendea haki Tz.
Kumbe ni bora tungeendelea kutawaliwa na wakoloni tungekuwa mbali sana! Yaliyoachwa na wakoloni yote yako wapi? Baada ya kuwafukuza kila kitu kikaisha!
ReplyDeleteTZ tuna keep left, mbona hili bus lipo tofauti? Nadhani hii siyo picha halisi, na hata mazingira siyakwetu....tunaomba ufafanuzi anko...
ReplyDeletembona ni lefthand drive anko...hii ni TZ kweli?
ReplyDeleteHuyo afande alikuwa naitwa afande "sharp" Mkama...
ReplyDeleteAu Sgt Mkama wakati ule. Alikuwa akitembea kama anacheza gwaride...
duh,watu wana macho makali kweli kweli.wanapekua mpaka matairi,bahati nzuri hakuna plate number.
ReplyDeleteJapokuwa haya maswali mawili hapo chini yameulizwa kwa anko Michuzi, naomba nijaribu kumsaida kuweza kuweka mambo sawa, tuweze kusaidiana uelewa.
ReplyDeleteSwali 1: TZ tuna keep left, mbona hili bus lipo tofauti? Nadhani hii siyo picha halisi, na hata mazingira siyakwetu....tunaomba ufafanuzi anko...
Ufafanuzi: Inawezekana hiyo picha si ya Tanzania, ILA kwa mtazamo wangu hili basi lipo sawa kabisa, lina-keep left kama magari mengine TZ ndio maana milango ya abiria ipo upande wa kushoto mwa basi. Alama za kwenye lami zisikuchanganye.
Swali 2: Mbona ni lefthand drive anko...hii ni TZ kweli?
Ufafanuzi: Upande wa dereva katika gari haumaanishi nchi linapoendeshwa hilo gari. Japokuwa magari mengi TZ ni Right Hand Drive (RHD), haimanishi hakuna magari Left Hand Drive (LHD), pia haimaanishi haiwekani kuendesha LHD ukiwa TZ.
Udhaifu wa hoja yako katika taaluma tunaita "faulty generalization" au wakati mwingine tunaita "fallacy of division".
SAMWELI.
Mi naona usukani upo kulia na upande wa kushukia ni sawia na driving system ya TZ. Ni muhimu kuleta mabasi hayo bila zengwe za kisiasa uchwara!
ReplyDeletekwa mliokuja leo Dar hii ndio aina ya usafiri tuliokuwa nao wenzenu...
ReplyDeleteWadau mnaouliza hayo mabasi kuwa lefthand ni kweli divyo yalivyokuja na ingawa sisi tunatumia righthand, lakini haya mabasi yalikuwa ni lefthand, ni kweli kabisa tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele kutokana na hali mbovu ya ubinafisishaji na kakithiri kwa rushwa na ulevi wa madaraka, kwani utaratibu wote tiliokuwa nao wakati huo umeachwa na wanaotuangusha ni viongozi wetu. Heri ya Mussa kuliko ya firauni.
ReplyDeleteKaka/dada unahangaika nini. Wengi wa wasiojua mambo ya Ikarus kumbakumba humu kwa Ankal wamekuja Dar baada ya miaka ya 90, hivyo usipate taabu wote hao ni "wa kuja"
ReplyDeleteJamani....jamani... Nyerere uko wapi jamani... uliteta haya mabasi kukomboa walala hoi. Leo wanashangaa. Kweli we ni wa kuota mbali kama alivyo jakaya leo. hakika akiondoka tutamkubuka sana jakaya anayefuata nyayo zako.... ah! Mchonga uko wapi jamani...
ReplyDeletelilikuwepo moja la rangi ya blue. Wakati nikisoma UDSM lilikuwa linakwenda Ubungo -Mwenge kupitia Chuo kikuu. Nililipa nick name ya academic Bus.
ReplyDeleteAsante kwa kumbukumbu nzuri. Anayesema haya mabasi yalikuwa wakati wa mkoloni arejee kusoma historia au aulize ndugu zake wakubwa. Haya mabasi yaliletwa kwenye miaka ya sabini mwanzoni.
Na kuwa left hand drive siyo sababu ya kusema kuwa hayakuwahi kuwa Tanzania. Nadhani tumechoka na matatizo ya nchi yetu hatutaki hata kufikiri.
Wadau mliouliza maswali:-
ReplyDelete1. Hapo barabarani ni kushoto kwa barabara kama tunavyoendesha sasa. Ila barabara ilikuwa nyembamba.
Angalia milango ya abiria iko upande gani.
2. Ndiyo Ikarus zote zilikuwa ni left hand drive. Hili bus lilikuwa la mwanzo kabisa katika majaribio kuona kama litawezekana kuendeshwa mitaa ya Dar. Ndio maana dereva mzungu, ambae pia aliwafundisha wazalendo.
3. Aliyesema tulikuwa tunasimamiwa na mapolisi kupanga foleni, nadhani ameingia Dar kwenye miaka ya 90s ..
Mimi sijawahi kuona hilo.
Ndio bwana enzi Za Ekarusi na daladala si mchezo.
ReplyDeleteMdau hapo juu anahoji kama hii picha ilipigwa Tanzania wakati basi limeandikwa Usafiri Dar es Salaam. Ubishi nao unachangia kuturudisha nyuma.
ReplyDeleteUfafanuzi kwa wenye mashaka na usafiri huu kuwapo Dar es Salaam.
ReplyDeleteInawezekana kabisa mahala hapa katika picha hii si Dar es Salaam. Ukweli ni kwamba kwa tuliokuwepo Dar enzi hizo tunashuhudilisha kuwepo kwa usafiri huu.
Mabasi haya yalikuwa yanaletwa kutoka Hungary tayari yana rangi na alama za UDA.
Nimekumbuka mbali sana, maskini nchi yangu imerudi nyuma sana tena sana.
ReplyDeleteIcarus zilikuwa left hand drive,
ReplyDeletepicha imepigiwa hungary wakati Yanapelekwa bandarini ili kusafirishwa kuja Tanzania,
acha lile lenye rangi ya blue/samawati, lilikuwepo lingine lilikuwa na michoro ya kutangaza vitanda na magodoro yanayotengenezwa na kampuni ya 'SUPER BANCO'
Hapo IKarus lilikuwa linatolewa Kiwandani nchini Hungary na kupelekwa Bandarini tayari kusafirishwa kuja Dar Es Salaam.
ReplyDeleteTunahitaji barabara maalumu sasa kwa sababu ya foleni kubwa Dar, otherwise ingekuwa miaka ya 80 ambapo kununua gari ulikuwa unahitaji kupata kibari cha state motors ilipelekea kusiwe na foleni
Sawa kabisa afande "Mkama Sharp" Ila naona wachangiaji wengi ni watu wakuja ndio maana wanaleta ubishi usio na maana.
ReplyDeleteTulishafikia hapa, sasa tumerudi nyuma 50 years. Mungu wasamehe walaafii wanaotumalizia taifa letu. Eti mheshimiwa anasimama bungeni na kumtetea mtu anayetutafuna kama mchwa au kiwavi jeshi. Tena siku hizi hawa wanaoitwa UDA, hata sheria za barabarani hawataki kufuata, wana kiburi kuliko mtu yeyote. Wameikamata serikali hata pakupumulia hakuna. Ukiona sehemu kuna trafic jam isiyoeleweka jua tu kuna UDA limetanua na kuleta adha hiyo..
ReplyDeleteKwa maoni yangu wanatakiwa wafute kabisa hilo jina UDA katika magari yao. Tuliokuwepo wakati ule tunakumbuka jinsi walivyokuwa wanatii sheria za barabarani hata kusaida traffic kwa kutumia vibasi vyao vidogo vya ISUZU kuwasaka wahalifu wa barabarani..
Hii Dr imejazwa na wengi wakuja na wakuletwa, haya mabasi yalikuwa ndio usafiri wa hii Dar, waliozaliwa miaka ya sabini na mwanzoni themanini, twaenda shule twapanda haya mabasi, wanaoleta maswali mengi ni wale wakuja na wakuletwa
ReplyDeleteDah nimekumbuka mbali sana wakati nikija likizo dar, nakumbuka kulipanda Ikarus niliporudi kwetu TA kila nilivyohadithia hakuna alienielewa kama wengi wasivyoelewa leo. Kutoka Ta nilikuja na treni daa Tanzania bhana ilikuwa poa sana..
ReplyDeleteasante blogger kwa picha hii, ni muda mrefu nimekuwa nikifanya utafiti wangu mtandaoni na kujiuliza maswali mengi sana kichwani, ni kwanini serikali isijiingize katika swala la usafiri wa mabasi yaendayo kasi na kuuboresha usafiri huu. Nimeona mabasi ya kisasa yaliopo Dubai ya mfano kama huu ambayo yanaweza kupakia abiria wengi kwa wakati mmoja bila adha yoyote. Pia ingetumia utaratibu wa kadi kama za benki kama mmoja wa watoa maoni alivyoeleza vizuri hapo juu. Mimi ni mwanafunzi wa chuo kimoja nchini uturuki, nchi yenye watu zaidi ya 75 milioni wameweza kukabili tatizo la usafiri istanbul na ankara, itakuwa sisi 45 milioni tunashindwa??? siku si nyingi nitaanzisha blog maalum kwa ajili ya kudadisi mambo kama haya kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu kwa kutumia fikra za wapenda maendeleo. Asanteni
ReplyDeleteNakumbuka UDA kulikuwa na mama mmoja wa kinyakyusa akisndesha mabasi jijini, tena haya mabasi yalinunuliwa mapya haya tusubiri tuone hayo yanayoenda kasi.
ReplyDelete