Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2014

    Acha tu! Sijui kwa nini tunaenda mbele hatua moja na kurudi hatua kumi nyuma!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2014

    "Soon I will be back never mind"

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2014

    Kumbe uda kulikuwa na madereva wazungu, au jamaa ni mshihiri au baniani?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2014

    Ohh Michuzi, unanikumbusha mbali sana wakati nchi yetu ilikuwa bado na mshikamano wa kweli na upendo!! Ufisadi ulikuwa bado haujakithiri, ndio maana hata kiongozi wa wakati huo anaonekana kama "Mtakatifu"!!

    Naomba uwe unaposti picha nyingi za nyuma ili japo tujitafakari na turudishe ule utu na ubinadamu na ujasiriamali tuliokuwa nao wakati ule, maana licha ya hali ya kiuchumi kuwa tete, wananchi walijitahidi kuziba pengo kwa kutengeneza nguo (Mwanza karibu na mwaloni), sabuni, viatu na kandambili, mafuta ya kujipaka (tuliweza kuuza nje ya nchi kama Zambia na Malawi). Haya yote yalifanyika licha ya wakati mwingine mkono wa dola kutumia nguvu za ziada bila ya ruhusa kutoka juu (uhujumu uchumi n.k.)

    Tusiporudia ujasiri wa wakati ule nchi inaondoka mbele ya macho yetu!!

    Ewe Muumba ibariki Tanzania bara na visiwani!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2014

    Zamani tulikuwa watu wastaarabu tulikuwa tunapanga mstari kuingia kwenye ekarusi siku hizi bho utafikiri mang'ombe. Hate it

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2014

    yarudishwe tena jamani yalikuwa mkombozi tena haya hayahitaji kuwa na viti vingi.watu wanasimama na wanaenea wengi. mradi tu yatengewe njia kama wanavyosema public transport itapewa kipao mbele. wanafikiria mambo makuuubwa eti mabasi yaendayo kasi wakati ni kiasi tu cha kurudisha kitu kilicholwisha tumika na kikaonekana kufanya kazi vizuri ila tu usimamizi ulizorota. ekarusi namba wani amini usiamini yakiingia matatau barabarani yatakuwa yamechukua nafasi ya daladala 6. vurugu na foleni zitapungua.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2014

    Nadhani huu Mpango wa Mabasi yaendayo Kasi Dart Jijini Darisalam wangerudusha tu mabasi haya yaliyokuwa ya UDA aina ya Ikarus tatizo la Usafiri lingekwisha!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2014

    Pia tiketi ya msimu yaani unakata tiketi ya basi la UDA ya mwezi mzima in-advance na unatumia kwa route zote za mabasi jijini DSM bila haja ya kulipia reja reja kila upandapo mabasi.

    Haikuwa tofauti na jinsi usafiri wa 'ulaya-ulaya' wa umma ulivyo sasa yaani tiketi za msimu za wakubwa na watoto(pamoja na wanafunzi), taimu tebo (time schedule) ya mabasi inajulikana kila baaada ya dakika ngapi basi litawasili katika kituo husika n.k
    Wazazi wanakununulua tiketi ya msimu inakuwa hakuna tena haja ya kuomba nauli kila asubuhi kuwahi shule.

    Kama mdau hapo juu alivyosema tumerudi hatua kumi mara mbili nyumba ktk masuala ya usafiri wa umma wa mijini.

    Mdau
    Christos Papachristou
    Diaspora

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2014

    Hiyo picha ya Ikarus haikupigwa Bongo , na huyo dereva ni M-Hungary

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 05, 2014

    Eti tulikua tunapanga foleni wenyewe? Alikuwepo afande wa pale msimbazi aliyepanda cheo kwa kusimamia foleni, jina limenitoka kidogo ila alikuwa maarufu kwa mikogo ya aina yake. Pia walikuwepo Wabulgaria wenye pistol vibindoni wakilinda foleni. Mdau kumbuka vizuri!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 05, 2014

    Haya mabasi bado yapo duniani na hata yalipotoka. Huku Marekani kwenye majimbo ya NewYork na miji mingine mikubwa where public transportation is the backbone for the means of going and come back from work.

    Is not true?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 05, 2014

    Taifa hili linahujumiwa na wale tulio waamini kuwapa madaraka watuongoze.
    Usafiri wa Dar hauhitaji bara bara maalumu.Tunahitaji nidhamu tu na usimamizi madhubuti.

    Tujitathimini tuijenge nchi yetu.Kizazi kijacho kitatulaumu sana kwa kutoitendea haki Tz.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 05, 2014

    Kumbe ni bora tungeendelea kutawaliwa na wakoloni tungekuwa mbali sana! Yaliyoachwa na wakoloni yote yako wapi? Baada ya kuwafukuza kila kitu kikaisha!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 05, 2014

    TZ tuna keep left, mbona hili bus lipo tofauti? Nadhani hii siyo picha halisi, na hata mazingira siyakwetu....tunaomba ufafanuzi anko...

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2014

    mbona ni lefthand drive anko...hii ni TZ kweli?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2014

    Huyo afande alikuwa naitwa afande "sharp" Mkama...
    Au Sgt Mkama wakati ule. Alikuwa akitembea kama anacheza gwaride...

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 05, 2014

    duh,watu wana macho makali kweli kweli.wanapekua mpaka matairi,bahati nzuri hakuna plate number.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 05, 2014

    Japokuwa haya maswali mawili hapo chini yameulizwa kwa anko Michuzi, naomba nijaribu kumsaida kuweza kuweka mambo sawa, tuweze kusaidiana uelewa.

    Swali 1: TZ tuna keep left, mbona hili bus lipo tofauti? Nadhani hii siyo picha halisi, na hata mazingira siyakwetu....tunaomba ufafanuzi anko...

    Ufafanuzi: Inawezekana hiyo picha si ya Tanzania, ILA kwa mtazamo wangu hili basi lipo sawa kabisa, lina-keep left kama magari mengine TZ ndio maana milango ya abiria ipo upande wa kushoto mwa basi. Alama za kwenye lami zisikuchanganye.

    Swali 2: Mbona ni lefthand drive anko...hii ni TZ kweli?

    Ufafanuzi: Upande wa dereva katika gari haumaanishi nchi linapoendeshwa hilo gari. Japokuwa magari mengi TZ ni Right Hand Drive (RHD), haimanishi hakuna magari Left Hand Drive (LHD), pia haimaanishi haiwekani kuendesha LHD ukiwa TZ.

    Udhaifu wa hoja yako katika taaluma tunaita "faulty generalization" au wakati mwingine tunaita "fallacy of division".

    SAMWELI.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 05, 2014

    Mi naona usukani upo kulia na upande wa kushukia ni sawia na driving system ya TZ. Ni muhimu kuleta mabasi hayo bila zengwe za kisiasa uchwara!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 05, 2014

    kwa mliokuja leo Dar hii ndio aina ya usafiri tuliokuwa nao wenzenu...

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 05, 2014

    Wadau mnaouliza hayo mabasi kuwa lefthand ni kweli divyo yalivyokuja na ingawa sisi tunatumia righthand, lakini haya mabasi yalikuwa ni lefthand, ni kweli kabisa tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele kutokana na hali mbovu ya ubinafisishaji na kakithiri kwa rushwa na ulevi wa madaraka, kwani utaratibu wote tiliokuwa nao wakati huo umeachwa na wanaotuangusha ni viongozi wetu. Heri ya Mussa kuliko ya firauni.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 05, 2014

    Kaka/dada unahangaika nini. Wengi wa wasiojua mambo ya Ikarus kumbakumba humu kwa Ankal wamekuja Dar baada ya miaka ya 90, hivyo usipate taabu wote hao ni "wa kuja"

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 05, 2014

    Jamani....jamani... Nyerere uko wapi jamani... uliteta haya mabasi kukomboa walala hoi. Leo wanashangaa. Kweli we ni wa kuota mbali kama alivyo jakaya leo. hakika akiondoka tutamkubuka sana jakaya anayefuata nyayo zako.... ah! Mchonga uko wapi jamani...

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 05, 2014

    lilikuwepo moja la rangi ya blue. Wakati nikisoma UDSM lilikuwa linakwenda Ubungo -Mwenge kupitia Chuo kikuu. Nililipa nick name ya academic Bus.
    Asante kwa kumbukumbu nzuri. Anayesema haya mabasi yalikuwa wakati wa mkoloni arejee kusoma historia au aulize ndugu zake wakubwa. Haya mabasi yaliletwa kwenye miaka ya sabini mwanzoni.
    Na kuwa left hand drive siyo sababu ya kusema kuwa hayakuwahi kuwa Tanzania. Nadhani tumechoka na matatizo ya nchi yetu hatutaki hata kufikiri.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 06, 2014

    Wadau mliouliza maswali:-
    1. Hapo barabarani ni kushoto kwa barabara kama tunavyoendesha sasa. Ila barabara ilikuwa nyembamba.
    Angalia milango ya abiria iko upande gani.
    2. Ndiyo Ikarus zote zilikuwa ni left hand drive. Hili bus lilikuwa la mwanzo kabisa katika majaribio kuona kama litawezekana kuendeshwa mitaa ya Dar. Ndio maana dereva mzungu, ambae pia aliwafundisha wazalendo.
    3. Aliyesema tulikuwa tunasimamiwa na mapolisi kupanga foleni, nadhani ameingia Dar kwenye miaka ya 90s ..
    Mimi sijawahi kuona hilo.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 06, 2014

    Ndio bwana enzi Za Ekarusi na daladala si mchezo.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 06, 2014

    Mdau hapo juu anahoji kama hii picha ilipigwa Tanzania wakati basi limeandikwa Usafiri Dar es Salaam. Ubishi nao unachangia kuturudisha nyuma.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 06, 2014

    Ufafanuzi kwa wenye mashaka na usafiri huu kuwapo Dar es Salaam.

    Inawezekana kabisa mahala hapa katika picha hii si Dar es Salaam. Ukweli ni kwamba kwa tuliokuwepo Dar enzi hizo tunashuhudilisha kuwepo kwa usafiri huu.

    Mabasi haya yalikuwa yanaletwa kutoka Hungary tayari yana rangi na alama za UDA.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 06, 2014

    Nimekumbuka mbali sana, maskini nchi yangu imerudi nyuma sana tena sana.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 06, 2014

    Icarus zilikuwa left hand drive,
    picha imepigiwa hungary wakati Yanapelekwa bandarini ili kusafirishwa kuja Tanzania,
    acha lile lenye rangi ya blue/samawati, lilikuwepo lingine lilikuwa na michoro ya kutangaza vitanda na magodoro yanayotengenezwa na kampuni ya 'SUPER BANCO'

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 06, 2014

    Hapo IKarus lilikuwa linatolewa Kiwandani nchini Hungary na kupelekwa Bandarini tayari kusafirishwa kuja Dar Es Salaam.

    Tunahitaji barabara maalumu sasa kwa sababu ya foleni kubwa Dar, otherwise ingekuwa miaka ya 80 ambapo kununua gari ulikuwa unahitaji kupata kibari cha state motors ilipelekea kusiwe na foleni

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 06, 2014

    Sawa kabisa afande "Mkama Sharp" Ila naona wachangiaji wengi ni watu wakuja ndio maana wanaleta ubishi usio na maana.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 06, 2014

    Tulishafikia hapa, sasa tumerudi nyuma 50 years. Mungu wasamehe walaafii wanaotumalizia taifa letu. Eti mheshimiwa anasimama bungeni na kumtetea mtu anayetutafuna kama mchwa au kiwavi jeshi. Tena siku hizi hawa wanaoitwa UDA, hata sheria za barabarani hawataki kufuata, wana kiburi kuliko mtu yeyote. Wameikamata serikali hata pakupumulia hakuna. Ukiona sehemu kuna trafic jam isiyoeleweka jua tu kuna UDA limetanua na kuleta adha hiyo..
    Kwa maoni yangu wanatakiwa wafute kabisa hilo jina UDA katika magari yao. Tuliokuwepo wakati ule tunakumbuka jinsi walivyokuwa wanatii sheria za barabarani hata kusaida traffic kwa kutumia vibasi vyao vidogo vya ISUZU kuwasaka wahalifu wa barabarani..

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 06, 2014

    Hii Dr imejazwa na wengi wakuja na wakuletwa, haya mabasi yalikuwa ndio usafiri wa hii Dar, waliozaliwa miaka ya sabini na mwanzoni themanini, twaenda shule twapanda haya mabasi, wanaoleta maswali mengi ni wale wakuja na wakuletwa

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 06, 2014

    Dah nimekumbuka mbali sana wakati nikija likizo dar, nakumbuka kulipanda Ikarus niliporudi kwetu TA kila nilivyohadithia hakuna alienielewa kama wengi wasivyoelewa leo. Kutoka Ta nilikuja na treni daa Tanzania bhana ilikuwa poa sana..

    ReplyDelete
  36. asante blogger kwa picha hii, ni muda mrefu nimekuwa nikifanya utafiti wangu mtandaoni na kujiuliza maswali mengi sana kichwani, ni kwanini serikali isijiingize katika swala la usafiri wa mabasi yaendayo kasi na kuuboresha usafiri huu. Nimeona mabasi ya kisasa yaliopo Dubai ya mfano kama huu ambayo yanaweza kupakia abiria wengi kwa wakati mmoja bila adha yoyote. Pia ingetumia utaratibu wa kadi kama za benki kama mmoja wa watoa maoni alivyoeleza vizuri hapo juu. Mimi ni mwanafunzi wa chuo kimoja nchini uturuki, nchi yenye watu zaidi ya 75 milioni wameweza kukabili tatizo la usafiri istanbul na ankara, itakuwa sisi 45 milioni tunashindwa??? siku si nyingi nitaanzisha blog maalum kwa ajili ya kudadisi mambo kama haya kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu kwa kutumia fikra za wapenda maendeleo. Asanteni

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 06, 2014

    Nakumbuka UDA kulikuwa na mama mmoja wa kinyakyusa akisndesha mabasi jijini, tena haya mabasi yalinunuliwa mapya haya tusubiri tuone hayo yanayoenda kasi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...