Na Sultani Kipingo
wa Globu ya Jamii
Siku ya tatu tu tokea michuano ya kombe la Dunia ianze nchini Brazil, tayari mabingwa watetezi Spain wanakuta kombe hilo linateleza mikononi mwao.
Japokuwa miaka minne iliyopita
walipoteza mchezo wao kwa kwanza dhidi ya Switzerland huko Afrika ya Kusini,
lakini hiyo haiwezi kulinganishwa na kilichotokea uwanja wa Fonte Nova katika mji wa Salvador ulio Kaskazini-Mashariki ya Brazil
usiku wa kuamkia leo baada ya kuchwapwa bao 5-1 na Holland.
Hilo ni pigo kubwa kwa Spain kupata tokea mwaka
1963 walipochabangwa na Scotland, ila safari hii aibu yake ni
maradufu kwa vijana hao wa kocha Vicente del Bosque. Ni sawa na matokeo ya
ndondi pale Tyson alipopigwa na kuvuliwa ubingwa Las Vegas. Wadadisi wanasema
ni timu chache zinaweza kuzinduka baada ya kipigo kama hicho. Sasa wanasubiri
kuona Spain itakuwaje.

Ukifikiria sana unajikuta unakubali kwamba kipigo
cha 5-1 ni janga kwa Spain, hasa ukizingatia ilianza kuongoza kwa bao 1-0 na
kuwa mbele kabla ya mapumziko. Saa moja baadaye Spain wakajikuta wanasujudu kwa
mabao hayo ambayo kama si kipa wao Iker Casillas kuokoa mikwaju mingine kibao ingekuwa
7-1 ama hata 8-1. Kitu pekee kilichowaokoa isiwe hivyo ni kipyenga cha mwisho…

Katika mchezo mwingine Chile imeifunga Australia bao 3-1 katika uwanja wa Pantanal Cuiba.
Leo timu ingine ya Afrika, Ivory Coast, inatupa karata yake ya kwanza kwa kucheza na Japan katika uwanja wa Pernambuco mjini Recife, wakati Enland inakipiga na Italy katika mchezo mwingine wa kukata na shoka katika uwanja wa Amazonia mjini Manaus.
Leo pia Columbia watacheza na Greece, wakati Uruguay itapambana na Costa Rica. Kuona muda wa kuanza michezo hiyo angalia ratiba hapo juu.
Kichapo cha kutisha lakini dont write the obituary yet, dont write them off.Hata hivyo kwangu man of the match must be Iker Casillais.Kama angeshindwa kuzuia mikwaju mingi mingine wengelala kwa mabao tisa.Kisha kumbuka kama angemwangusha Van Persie,angepigwa red card na Spain wengecheza dakika ishirini za mwisho bila kipa wao.
ReplyDelete