Mama Maria Nyerere akitoa nasaa wakati wa Ufunguzi wa Semina kwa Wanawake Wajasiliamali kutoka Mikoa yote ya Tanzania, akiwa ni Mwanamke Mjasiliamali pia, amewahakikishia wanawake mafanikio iwapo watajiamini na kumsirikisha Mungu katika kazi zao.
Mwenyekiti wa EOTF Mama Anna Mkapa, akitoa utangulizi wa Mafunzo na ntambulisho wa Waalikwa, wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu kwa Wanawake Wajasiliamali, kuanzia Juni 23-25/2014, kuanzia saa2 asubuhi katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani jijini Dares Salaam.Picha na Maelezo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote(EOTF), Ndugu, Stephen Emmanuel akimkaribisha Mwenyekiti wa EOTF, Mama Anna Mkapa (hayuko pichani) leo, tarehe 23/06/2014 wakati wa Ufunguzi wa Semina kwa Wanawake Wajasiliamali kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar. Mafunzo hayo yanalenga kumsaidia Mwanamke kukabiliana na changamoto za Ujasiliamali.
Wanawake kutoka Mikoa Mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar wakiwa katika Ufunguzi wa Semina ya Mafunzo ya Wajasilaimali, Mafunzo ni ya muda wa siku tatu kuanzia Juni 23-25/2014, kuanzia saa2 asubuhi katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani jijini Dares Salaam.
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa IPP, Dkt. Reginald Mengi (aliayevaa Suti) akiwasili katika Ufunguzi wa Semina ya Mafunzo kwa Wanawake Wajasiliamali, Mbele ya Msafara ni Mama Maria Nyerere na Mwenyekiti wa EOTF Mama Anna Mkapa. Semina kwa Wajasiliamali imeandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa Kwa wote(EOTF), Mafunzo ni ya muda wa siku tatu kuanzia Juni 23-25/2014, kuanzia saa2 asubuhi katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani jijini Dares Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...