Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa Mtoto Mosi Kimosa ,7, anayesoma darasa la pili katika shule ya msingi Msimba iliyoko Kigoma Vijijini na Trisa Luziga,6, anayesoma darasa la kwanza mara baada ya Mama Salma kutua katika uwanja wa ndege wa Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mheshimiwa Issa Machibya akimpokea rasmi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma Mama Salma yuko mkoani humo kuhudhuria maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu salama duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani Kigoma leo
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma za utamaduni zilizokuwa zikichezwa na akinamama wa Kigoma wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma kushiriki maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu salama duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani humo leo. Picha na John Lukuwi.
Kwa picha zaidi ya siku hiyo BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi ya siku hiyo BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...