Na Francis Dande
MAMIA ya
wakazi wa Jiji la Dar es Salaam
na vitongoji vyake, wakiwemo wanamichezo, leo wamejitokeza katika mazishi ya
bondia wa zamani wa masumbwi ya kulipwa, Iraq Hudu (49).
Marehemu Hudu, maarufu
kama ‘Kimbunga’, aliyefariki dunia Ijumaa mjini Dar es
Salaam , amezikwa leo majira ya saa 10:00 alasiri katika makaburi
ya Kisutu, jijini Dar es Salaam .
Bondia huyo
aliyewahi kutamba vilivyo katika ulingo wa masumbwi, alifariki alfajiri ya
Ijumaa katika hospitali ya Hindu Mandal, akisumbuliwa na tatizo la ini na figo
kutofanya kazi.
Hudu
alizaliwa mwaka 1965 Ujiji Kigoma, na kupata elimu ya msingi mkoani humo na
baadae kuja Dar es Salaam ambako alipata elimu ya sekondari. Baada ya
hapo, alijiingiza katika masumbwi katika miaka ya 1990 hadi miaka ya 2000,
alipoacha. Marehemu
ameacha watoto watatu.
Mwili wa Iraq Hudu ukishushwa katika gari maalumu wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Baadhi wa waombolezaji
wakiwa wamebeba jenza lililokuwa na mwili wa bondia wa zamani wa ngumi za
kulipwa Iraq Hudu ‘Kimbunga’ wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana katika
makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mazishi ya bondia Iraq Hudu yakifanika leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
inalilah wainailayhi rajiun... Ndo mwisho wa kila binadamu
ReplyDelete