Kocha wa Marekani ambaye ni mshambuliaji nyota wa zamani wa Ujerumani Jurgen Klinsmann na wachezaji wake wakishangilia bao la kwanza lililofungwa sekunde ya kwanza na Clint Dempsey pichani chini
Goli la dakika ya kwanza lililowekwa kimiani na Clint Dempsey na lingine la dakika za lala salama la rizevu John Brooks katika mchezo  uliopigwa usiku uliopita mjini Natal, Brazil,  ni magoli ambayo yameiwezesha Marekani kulipiza kisasi dhidi ya Ghana waliowafunga 2-1 na kuwafungasha virago mapema katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 Afrika ya Kusini
Ushindi huo unaiweka Marekani  katika nafasi ya pili ya kundi G nyuma ya Ujerumani. Marekani inafundishwa na mshambuliaji nyota wa zamani wa Ujerumani Jurgen Klinsmann. Ghana na Ureno ya Cristian Ronaldo wanachechemea kwa kila mmoja kutokuwa na pointi hadi sasa.
Likiwekwa kimiani katika sekunde 29 tu za mchezo, bao la Dempsey lilikuwa la tano kwa kufungwa mapema katika historia ya kombe la dunia, katika orodha ya mabao inayoongozwa na Hakan Sukur wa Uturuki aliyefunga dakika ya 11 dhidi ya Korea mwaka 2002.
Wakionekana kupagawa kwa goli hilo la mapema, Ghana walijitahidi kujiweka sawa, lakini kipa Tim Howard wa Marekani alikuwa makini.
Kukiwa kumesalia dakika nane mpira kumalizika, Andrea Ayew alisawazisha kwa bao tamu, pale alipopokea pasi ya nyuma toka kwa Asamoah Gyan, kabla ya kumtungua Howard kwa shuti la nje ya mguu.
Hata hivyo Marekani hawakukatishwa tama, pamoja na kuchezewa nusu uwanja kwa muda mwingi dakika za lala salama, Brooks aliyeingia kipindi cha pili alitingisha nyavu kwa kichwa baada ya majalo tamu ya kona toka kwa Graham Zuzi.
Angalia Hakan Sukur wa Uturuki akiweka mpira kimiani dakika ya 11 na kuweka rekodi ya bao la haraka katika Kombe la Dunia dhidi ya Korea mwaka 2002.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2014

    Dakika ya 11 haliwezi kuwa bao la mapema labda sekunde ya 11

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...