Kocha wa Marekani ambaye ni mshambuliaji nyota wa zamani wa Ujerumani Jurgen Klinsmann na wachezaji wake wakishangilia bao la kwanza lililofungwa sekunde ya kwanza na Clint Dempsey pichani chini
Goli la dakika ya kwanza lililowekwa kimiani na Clint
Dempsey na lingine la dakika za lala salama la rizevu John Brooks katika mchezo
uliopigwa usiku uliopita mjini Natal,
Brazil, ni magoli ambayo yameiwezesha Marekani kulipiza
kisasi dhidi ya Ghana waliowafunga 2-1 na kuwafungasha virago mapema katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010
Afrika ya Kusini
Ushindi huo unaiweka
Marekani katika nafasi ya pili ya kundi
G nyuma ya Ujerumani. Marekani inafundishwa na mshambuliaji nyota wa zamani wa
Ujerumani Jurgen Klinsmann. Ghana na Ureno ya Cristian Ronaldo wanachechemea
kwa kila mmoja kutokuwa na pointi hadi sasa.
Likiwekwa kimiani katika
sekunde 29 tu za mchezo, bao la Dempsey lilikuwa la tano kwa kufungwa mapema
katika historia ya kombe la dunia, katika orodha ya mabao inayoongozwa na Hakan
Sukur wa Uturuki aliyefunga dakika ya 11 dhidi ya Korea mwaka 2002.
Wakionekana kupagawa kwa goli
hilo la mapema, Ghana walijitahidi kujiweka sawa, lakini kipa Tim Howard wa
Marekani alikuwa makini.
Kukiwa
kumesalia dakika nane mpira kumalizika, Andrea Ayew alisawazisha kwa bao tamu,
pale alipopokea pasi ya nyuma toka kwa Asamoah Gyan, kabla ya kumtungua Howard
kwa shuti la nje ya mguu.
Hata hivyo Marekani
hawakukatishwa tama, pamoja na kuchezewa nusu uwanja kwa muda mwingi dakika za
lala salama, Brooks aliyeingia kipindi cha pili alitingisha nyavu kwa kichwa
baada ya majalo tamu ya kona toka kwa Graham Zuzi.
Angalia Hakan Sukur wa Uturuki akiweka mpira kimiani dakika ya 11 na kuweka rekodi ya bao la haraka katika Kombe la Dunia dhidi ya Korea mwaka 2002.
Angalia Hakan Sukur wa Uturuki akiweka mpira kimiani dakika ya 11 na kuweka rekodi ya bao la haraka katika Kombe la Dunia dhidi ya Korea mwaka 2002.
Dakika ya 11 haliwezi kuwa bao la mapema labda sekunde ya 11
ReplyDelete