Afisa kutoka TASAF makao makuu Bw. Geodfrey
Nyamwihula akisisitiza jambo kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini
katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati walengwa wa
mpango huo walipopewa mafunzo ya namna ya kuibua miradi ya ujenzi PWP ambayo ni
moja ya jitihada za serikali kupitia TASAF kuongeza pato la kaya husika .
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeanza zoezi la
kuwashirikisha walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini kuibua miradi ya
Ujenzi PWP ambayo kwa mujibu wa taratibu walengwa watatumia fursa ya kufanya
kazi katika miradi watakayoibua kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira ambao
utasaidia kuwaongezea kipato.
Walengwa watafanya kazi hiyo kwa kipindi cha siku
15 katika mwezi na siku 60 kwa mwaka hususani wakati wa kipindi cha hari
(kipindi kigumu).Chini ya utaratibu huo asilimia 75 ya fedha zitalipwa kwa
walengwa na 25 zitatumika kununua vifaa vitakavyotumika kwenye mradi husika.
Mwezeshaji wa Mpango wa uibuaji miradi ya Ujenzi
Issa Jabri akitoa maelezo ya namna ya kuibua miradi ya ujenzi PWP katika shehia
ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Pichani walengwa wa PWP katika shehia ya Mpapa
wakisikiliza maelezo kutoka kwa mwezeshaji (hayupo pichani) juu ya namna ya
uibuaji wa miradi kwenye eneo lao.

Mwezeshaji wa PWP katika shehia ya Kipange,huko Unguja Bi. Hidaya Mussa akitoa maelezo ya namna ya kuibua Miradi ya Ujenzi PWP kwa walengwa wa mpango huo .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...