Na Woinde Shizza, Manyara
Kinyanganyiro cha kugombea Redd's Miss Manyara 2014, kinatarajia
kufanyika kesho Jumamosi Juni 14 mwaka huu katika ukumbi wa CCM Mkoa, mjini Babati,
ambapo warembo 10 wanatarajia kuchuana.
Mkurugenzi wa Mirerani Entertainment, Akon Clement ambaye ni Mratibu
wa mashindano hayo alisema mgeni rasmi wa mashindano hayo anatarajiwa
kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Mary Nagu.
Akon alisema msanii maarufu wa kizazi kipya, Bob Junior kutoka jijini
Dar es salaam anatarajiwa kutoa burudani kali wakati akisindikiza
michuano hiyo ambapo pia wasanii chipukizi kutoka mjini Babati
watashiriki kunogesha.
Aliwataja wanyange hao wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kuwa ni
Miss Mirerani 2014 Amina Omary, Miss Mirerani namba mbili Catherine
Emmanuel na Miss Mirerani namba tatu Happy William.
Wengine ni Fatuma Salim, Betha Fredrick, Rose Evason, Edna Mushi,
Hosiana John, Mary Ruta na Flora Godlizen, ambao ni warembo
walioshinda kwenye mashindano ya wilaya za Babati, Hanang' na Mbulu, alisema Clement.
Aliwataja wadhamini wa mashindano hayo ni kampuni ya Tanzania
Breweries (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd's Original, Open
University, Manyara Computer, mireranitanzanite.blogspot.com,libeneke
la kaskazini blog na Active Classic Fashion.
Mratibu huyo alisema kuwa wadhamini wengine wa shindano hilo ni
TanzaniteOne, Assey Printing company, Trimus Saloon, Kifaru Agrovet,
Winners Hotel, Sarafina Lodge na Kimweri Sport Wear.
Warembo wanaogombania Miss Manyara 2014
Warembo wanaogombania Miss Manyara 2014 wakiwa wanacheza mmoja ya wimbo watakaoucheza katika siku ya mashindano ikiwa ni moja ya sehemu ya mazoezi. Picha na Woinde Shizza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...