Na Mwandishi Wetu

Promosheni ya Kwea Pipa na televisheni ya Taifa ya TBC  kwa kushirikiana na kampuni ya Push Mobile Media Limited imezidi kupamba moto baada ya mshindi mmoja zaidi kupatikana.

Deocary Mkenda ambaye ni mkazi wa Sinza ameungana na wenzake wawili ambao wamekwisha zawadiwa tiketi zao na sasa kampuni ya Push Mobile Media Limited inawatafutia pasipoti kwa ajili ya kusafri na kuona mechi ya Brazil na Cameroon Juni 23 mjini Rio de Janeiro.

Mkenda (35) ambaye ni Mhasibu katika kampuni ya Ernst & Young ya jijini anaungana na Donald Milinde Shija (34) mkazi wa Mabibo jijini ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Davis and Shirtliff na mshindi mwingine ni Shaban Athumani Saidi (22) mkazi wa Banana-Kitunda.

Meneja kampeni wa promosheni hiyo ya Semu Bandora alisema kuwa bado tiketi mbili kwa ajili ya mashabiki wa soka nchini ili kujishindia tiketi kwa ajili ya kuona kombe hilo.

Bandora alisema kuwa droo nyingine itafanyika wiki ijayo na lengo ni kuona mashabiki wanapata fursa hiyo ya kuona mashindano hayo makubwa kabisa ya soka duniani.

“Tunawaomba mashabiki wa soka kuendelea kushiriki katika promosheni hii ili kupata nafasi ya kuwaona mastaa wa dunia kama akina Benoit Assou-Ekotto, Alex Song na Samuel Eto’o na yule wa  Brazil kama vile Neymar da Silva Santos Júnior, Thiago Silva, Dan Alves na wengine wengi,” alisema Bandora.

Alisema kuwa mbali ya tiketi za kombe la dunia, pia kuna zawadi za ving’amuzi zaidi ya 250, televisheni za flat screen sita na fedha taslimu ambazo zote zimeandaliwa kwa ajili ya kuwazawadia mashabiki wa soka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...