Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifungua rasmi Mkutano wa wadau
wa Huduma ya Afya ya Msingi (PHC - Primary Health Care) kwa Wananchi
Mkoani Rukwa tarehe 30 Mei 2014 katika ukumbi wa RDC mjini Sumbawanga.
Katika kikao hicho mambo mbalimbali ya msingi kuhusu afya ya jamii
yalijadiliwa na kuwekewa mpango kazi wa utekelezaji katika kuimarisha
afya ya jamii Mkoani Rukwa. Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja
na mkakati wa kupunguza vifo vya mama wajawazito, maendeleo ya shughuli
za usafi wa mazingira, utekelezaji wa shughuli za chanjo ya magonjwa
mbalimbali, utaratibu wa utoaji wa PF 3, hali ya homa ya Dengu na
lishe.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Manyanya akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mkutano huo. Katika salam zake za ufunguzi alisisitiza juu ya usafi wa
mazingira ambao ndio kinga kuu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo ya
kuambukiza kama Dengu na magonjwa ya mlipuko. Aliupongeza mpango wa
Sumbawanga Nga'ara ambao kwa kiwango kikubwa umeleta mabadiliko ya usafi
katika mji wa Sumbawanga tofauti na siku za nyuma. Aliipongeza pia
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa hatua waliyofikia wa kuagiza
magari mawili ya kubebea taka yatakasaidia katika kuimarisha mpango huo
wa usafi katika Manispaa ya Sumbwanga na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akiwasilisha mada ya hali ya
huduma ya afya ya mama, baba na mtoto Mkoani Rukwa katika mkutano huo.
Mwanasheria
Mfawaidhi wa Serikali Mkoa wa Rukwa Msomi Prosper Rwegerera
akiwasilisha mada ya utaratibu wa utoaji wa PF 3 kwa mtu alijeruhiwa.
Alisema PF 3 ni muhimu katika ushahidi wa kimahakama pale mtu
atakapokuwa anadai haki yake mahakamani kutokana na jeraha aliliopata na
pia inakuwa ni kithibitisho cha kisheria kwa kilichotokea kwa majeruhi
husika. Katikati ni Afsa Afya wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Kenedy Kyauke.
Sehemu ya wadau wa Mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa kwa umahiri mkubwa. Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com
Sana sana, kinga ya mwanzo iwalenge walalahoi; sio wafanyakazi wajua Kiingereza!
ReplyDeleteSemina za namna hiyo ziendeshwe kwa Kiswahili; tuachane na Kiingereza, jamani!
Nijuavyo mie hizo semina huendeshwa kwa lugha ya kiswahili kwa wadau ambao wana ushawishi mkubwa kwa watu wao, wakiwemo viongozi wa dini, wataalam wa afya na wanasiasa pia ambao baadae hufikisha elimu hizo kwa jamii inayowazunguka. Kwahiyo usisemee kitu ambacho hukijui just let it go hutopoteza kitu, no research no right to speak Mr. Annonymus
DeleteNani kakwambia semina hiyo iliiendeshwa kizungu acha kuropoka! kitu kama hukijui piga kimya. No research no right to speak.
ReplyDeletePicha ya tatu kutoka juu kuna mtu anawasilisha mada. Hapo katika slide anazotumia ni wazi hicho ni kiingereza ndo maana mdau anasema hata hizo "slides" zinatakiwa ziwe kwa kiswahili.
ReplyDeleteObserver