Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifungua rasmi Mkutano wa wadau wa Huduma ya Afya ya Msingi (PHC - Primary Health Care) kwa Wananchi Mkoani Rukwa tarehe 30 Mei 2014 katika ukumbi wa RDC mjini Sumbawanga. Katika kikao hicho mambo mbalimbali ya msingi kuhusu afya ya jamii yalijadiliwa na kuwekewa mpango kazi wa utekelezaji katika kuimarisha afya ya jamii Mkoani Rukwa. Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na mkakati wa kupunguza vifo vya mama wajawazito, maendeleo ya shughuli za usafi wa mazingira, utekelezaji wa shughuli za chanjo ya magonjwa mbalimbali, utaratibu wa utoaji wa PF 3, hali ya homa ya Dengu na lishe. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Manyanya akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Katika salam zake za ufunguzi alisisitiza juu ya usafi wa mazingira ambao ndio kinga kuu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kuambukiza kama Dengu na magonjwa ya mlipuko. Aliupongeza mpango wa Sumbawanga Nga'ara ambao kwa kiwango kikubwa umeleta mabadiliko ya usafi katika mji wa Sumbawanga tofauti na siku za nyuma. Aliipongeza pia Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa hatua waliyofikia wa kuagiza magari mawili ya kubebea taka yatakasaidia katika kuimarisha mpango huo wa usafi katika Manispaa ya Sumbwanga na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akiwasilisha mada ya hali ya huduma ya afya ya mama, baba na mtoto Mkoani Rukwa katika mkutano huo.
Mwanasheria Mfawaidhi wa Serikali Mkoa wa Rukwa Msomi Prosper Rwegerera akiwasilisha mada ya utaratibu wa utoaji wa PF 3 kwa mtu alijeruhiwa. Alisema PF 3 ni muhimu katika ushahidi wa kimahakama pale mtu atakapokuwa anadai haki yake mahakamani kutokana na jeraha aliliopata na pia inakuwa ni kithibitisho cha kisheria kwa kilichotokea kwa majeruhi husika. Katikati ni Afsa Afya wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Kenedy Kyauke.
Sehemu ya wadau wa Mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa kwa umahiri mkubwa. Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2014

    Sana sana, kinga ya mwanzo iwalenge walalahoi; sio wafanyakazi wajua Kiingereza!

    Semina za namna hiyo ziendeshwe kwa Kiswahili; tuachane na Kiingereza, jamani!

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJune 01, 2014

      Nijuavyo mie hizo semina huendeshwa kwa lugha ya kiswahili kwa wadau ambao wana ushawishi mkubwa kwa watu wao, wakiwemo viongozi wa dini, wataalam wa afya na wanasiasa pia ambao baadae hufikisha elimu hizo kwa jamii inayowazunguka. Kwahiyo usisemee kitu ambacho hukijui just let it go hutopoteza kitu, no research no right to speak Mr. Annonymus

      Delete
  2. AnonymousJune 01, 2014

    Nani kakwambia semina hiyo iliiendeshwa kizungu acha kuropoka! kitu kama hukijui piga kimya. No research no right to speak.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 02, 2014

    Picha ya tatu kutoka juu kuna mtu anawasilisha mada. Hapo katika slide anazotumia ni wazi hicho ni kiingereza ndo maana mdau anasema hata hizo "slides" zinatakiwa ziwe kwa kiswahili.

    Observer

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...