Mtoto Nasrah Rashid, aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua na kupata ulemavu kwa kufungiwa kwenye boksi miaka minne amefariki dunia leo na kuacha huzuni kubwa miongoni mwa wananchi wakiosikia mkasa wake wa kusikitisha. 
 Nasra alifichwa kwenye boksi na mama yake mkubwa aitwaye Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro tangu akiwa na miezi tisa baada ya mama yake mzazi kufariki dunia.
Bw. Rashid Mvungi akimuangalia mtoto wake Nasrah Rashid (4) ambaye ni mlemavu wa viungo aliyefungiwa chumbani na kufichwa kwenye boksi bila ya kufanyiwa usafi tangu akiwa na umri wa miezi tisa.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2014


    R.I.P mtoto Nasra
    Mwenyezi Mungu akulaze mahali pema
    utakumbukwa daima kwa mateso uliyoyapata miaka minne.

    Mikidadi-Denmark

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2014

    R.I.P Nasra.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 02, 2014

    Yaa Allah, umfanye mtoto huyu kuwa mwokozi wetu na mwenye kukubaliwa dua yake na umpe pepo isio na mpaka , ikiwa kifo chake ni ahadi au kimesababishwa na watu au mtu wewe ndiye mjuzi wa hilo na mwepesi wa kuhukumu na mwadilifu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 02, 2014

    Ee mungu tupe roho za huruma tupendane. Unyama kama huu tupe nguvu tuukemee inauma na kusikitisha sana mwanamke kuwa na roho ya kinyama hivi pumzika kwa amani mwanangu mwenyezi mungu akulaze mahala pema peponi amen xx

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 02, 2014

    Kalale kwa amani Nasra baada ya mateso uliyoyapata Mola alikudhirisha kwa umma ili upate kuona upande wa pili ya wanaadamu wenye huruma angalau kwa siku chache. Nenda mwanetu kwa Mola ambaye ni Mkarimu zaidi kuliko sisi daima tutakukumbuka kwa bashasha zako hata baada ya kupitia magumu. Habari zako zilituhuzunisha mno lakini zimetuachia mafunzo na ujumbe mzito wa kuzidi kuwahurumia watoto. Inna Lillahi wainna ilayhi raajiuun

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 02, 2014

    Eti akimwangalia mtoto wake!!!!! Yaani huyo jamaa ni baba wa huyu mtoto au sijaelewa jamani?????? Nasiki Alikuwa wapi huyu! AU nimeosea kusoma! Yaani Mungu atawarudishia wanayostahili! Mtoto huyu ni Malaika anapumzika na malaika wengine kwa raha sasa!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 02, 2014

    Kwa hiyo huyu baba anakabiliwa na mashtaka ya mauaji bila kukusudia? Adhabu yake ni miaka mingapi?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 02, 2014

    How can somebody do that to a beautiful child, her days are coming where she pay what she did.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 02, 2014

    Allah akupe janatul wanaimu na uwe muokozi na mtetezi kwatu sote siku ya malipo(Kiama), pomoja na wazazi wako wawili. Tulikuhurumia sana kwa mateso uliyoyakabili muda wote ukiwa ndani ya Jela ya Box. Hakika nasfsi zetu zimeguswa sana sana mpaka tunashindwa kuelezea.

    Wazazi tuwaonene huruma malaika wa mungu kwani wao hawana hatia.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 02, 2014

    Wapendwa habari ya mtoto huyu kila siku inaniuma sana. kumbe baba yake mzazi alikuwepo? sikuzote mtoto alizofungiwa alikuwa wapi? kwa nini hakumtafuta mtoto wake? ni maswali kila mara huwa najiuliza japo sipati majibu. Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi, tulikupenda Nasrah, ila mapenzi yake yatimizwe.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 02, 2014

    pumzika kwa amani sasa ukijua safari yako yenye makali haya imekwisha. Kwa Mungu atahakisha mateso yako yanapoa. Sisi tutamwombea Mama yako mkubwa kwani hatuwezi mhukumu, kwa maana mola tu ndiye anayeelewa kitendawili hiki. Tunamuombea apate anachokistahili kama Mungu aonavyo....kwa wote waliompenda na kumtunza kwa upendo hadi mauti ya Nasra, Mungu awazidishie baraka tele. Lala mtoto Nasra lala salama

    ReplyDelete
  12. nimeumia jamani mpaka nimelia,sina budi kumshukuru mungu kwa yote,ninakupenda nasra nilitamani nikuone siku moja.ulikuwa ni mtoto mzuri wa kupewa malezi mazuri yanayostahili.pumzika kwa amani nasra tunamuachia mungu yeye ndiye atakaetoa hukumu inayostahili kwa wale wote waliokufanyia ukatili huu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...