MWENYEKITI TAWI LA CCM MOSCOW URUSI, NDG SALIM MFUNGAHEMA: 

 Mwenyekiti tawi la CCM Moscow Ndg Mfungahema Salim amesema muundo wa muungano wa serikali Mbili ndio suluhisho pekee la watanzania, Akizungumza katika kikao cha kamati ya siasa ya tawi kilichofanyika 05.06.2014, bwana Mfungahema alisema muungano wa serikali mbili ndio umetufikisha hapa tulipo na kuna mafanikio makubwa TULIYOYAPATA, pamoja na changamoto chache zinazojitokeza lakini zinarekebishika.

 Bwana Mfungahema aliwataka vijana wa CCM kuendelea kuungamkono muungano wa serikali mbili kwani ndio muungano wenye tija kwa taifa. Bwana Mfungahema alisema serikali tatu ni mzigo kwa taifa na hivyo hatunabudi kuendelea na mfumo wa serikali mbili na ikibidi tuelekee kwenye serikali moja kwani ni muungano sahihi na utaleta tija na mshikamano zaidi kwa watanzania. Pia mwenyekiti alimshukuru Mh Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa jitiada zake za kuwaletea maendeleo watanzania na kuboresha utawala bora Tanzania na Afrika kwa ujumla.

 Mh mwenyekiti Ndg SalimMfungahema alitumia fursa hiyo pia kumpongeza Mh Rais Kikwete kwa kupata tunzo la kuwa kiongozi bora barani Afrika mwenye mchango mkubwa wa kuleta maendeleo, amani na utawala bora, bwana Mfungahema alisema Rais Kikwete ametupatia heshima kubwa watanzania kote duniani.

   Kuhusu uchaguzi wa mwaka 2015, bwana Mfungahema alisema CCM inatarajia kupata ushindi mkubwa na wa kishindo mwaka 2015 kwa sababu CCM imetekeleza ilani yake ya uchaguzi vizuri na kwa wakati, na hivyo kuwafanya wananchi wawe na imani kubwa na CCM.

   Mwenyekiti pia alimpongeza katibu mkuu wa CCM MH Abdulrahmani Kinana kwa mchango wake mkuwa na kuimalisha chama, na kukipa cha uhai mkubwa na kurudisha imani ya wananchi kwa CCM, alisema jukumu la kuimalisha chama ni la kila mwana CCM na sio viongozi pekee, hivyo alitoa wito kwa vijana wanaporudi nyumbani Tanzania kutoa ushirikiano wa kuimarisha chama katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kuelezea jinsi ilani inavyotekelezeka.

                                KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
                               IMETOLEWA NA KATIBU WA TAWI
                              NDG HASSANI KAPILIMA, CCM MOSCOW.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2014

    Bora serikali 4(nne),maana sisi wapemba tutajitawala wenyewe na maamuzi yetu tutayafanya Pemba badala ya kuamuliwa Unguja.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2014

    ziwe 5,hata na sisi tumbatu tumechoka kuamuliwa mambo yetu na unguja

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2014

    serekali moja ndio jibu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...