Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wapili kulia) katika Banda la Nida kujifunza
masuala mbalimbali ya kiutendaji yanayofanywa na Mamlaka hiyo iliyopo Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Habari wa Wizara hiyo,
Christina Mwangosi.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia)
akimsikiliza kwa makini Afisa Tawala Mwandamizi wa Idara ya Wakimbizi, Jenita
Ndone wakati alipokuwa anaeleza majukumu ya Idara hiyo ambayo inasimamia
masuala ya wakimbizi nchini, wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
yanayoendelea katika Viwanja vya Manzi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto) akimuuliza
maswali Afisa wa Idara ya Uhamiaji, Mathew Ikomba kuhusu matatizo mbalimbali
likiwemo baadhi ya wananchi wanailalamikia Idara hiyo kuhusu uombwaji wa rushwa
wakati wanapoomba kupatiwa Hati ya Kusafiria (pasipoti). Malemi aliitaka idara
hiyo ifuate haki wakati wananchi wanapoomba pasipoti. Wizara na Idara zake
inashiriki katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam
Koplo
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Loyce
Abeid, akimuonyesha Naibu Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto) kifaa
kinachotumika kwa ajili ya uokozi wa magari yanapopata ajali hasa magari ya
tenki. Malemi alitetembelea Banda la Wizara na Taasisi zake katika Maonyesho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini
Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wapili kushoto
aliyekaa kwenye kiti) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wizara
yake ambao wapo katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kushoto aliyekaa kwenye kiti ni
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...