Mtendaji Mkuu wa Barclays PLC, Anthony Jenkins akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC Tanzania wakati wa ziara yake nchini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Bi. Mizinga Melu.
Mtendaji Mkuu wa Barclays PLC, Anthony Jenkins (kulia) akipozi kwa picha na Rachel Mwalukasa mmoja wa wafanyakazi aliyemkabidhi tuzo kwa kuwa mfano wa kuigwa katika suala la kujitolea binafsi katika kuisaidia jamii. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji nwa NBC Tanzania, Mizinga Melu.
Wafanyakazi wa NBC Tanzania wakionyesha sura ya matumaini wakati wakimsikiliza bosi wao, Antony Jenkins alipokuwa akizungumza kuhusu mikakati ya kimaendeleo ndani ya benki hiyo nchini.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC wakishangilia hotuba ya Mtendaji Mkuu wa Barclays PLC, Anthony Jenkins wakati wa ziara yake nchini Tanzania.
Mtendaji Mkuu wa Barclays PLC, Anthony Jenkins (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bytrade Tanzania Managing Director, Harish Dhutia katika hafla iliyoandaliwa na NBC kwa ajili ya wateja wa makampuni wakati wa ziara yake nchini Tanzania mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Mizinga Melu.
Wafanyakazi wa NBC Tanzania wafuatilia kwa makini hotuba ya Mtendaji Mkuju wa Barclays PLC, Anthony Jenkins wakati wa ziara yake nchini ambapo alifanya mikutano na wafanyakazi, wateja wa NBC na wadau wengine wa benki hiyo.
Ninampongeza sana dada Rahel (Recho) Mwalukasa kwa kuendeleza ufanyakazi uliotukuka. Huyu dada akiwa Barclays proper kabla haijanunua NBC alikuwa anapata zawadi za ufanyakazi bora na kupewa hadi treat Dubai. Leo hii alihamia NBC ambayo later Barclays waliinunua na ameendelea kuwa role model. Kwa hakika CRDB walimkosa na sielewi ni kwa nini MD. Kimei alishindwa kum-maintain. Keep it up dada Rahel.
ReplyDelete