Abiria wakiwa wanashangaa Daladala zinapita kituo cha Mwenge jijini Dar es salaam bila kusimama, ikiwa ni siku ya kwanza wasafirishaji hao kuamriwa kutumia kituo cha Makumbusho ambacho inaelekea hawaafiki.
 Daladala zikiwa zinapita bila kusimama sehemu yoyote
 Kituo cha kwenda Tegeta , Kawe na Mbezi kikiwa Kitupu Muda huu
 Kituo cha Mabasi Mwenye Cheupe hakuna hata Daladala hata moja
 Bajaji ndizo zimegeuka kuwa daladala na ni Tsh 1000 tu kwa mtu mmoja mpaka Mwenge
 Eneo ambalo Daladala zilikuwa nyingi sasa hakuna tena mabasi hayo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2014

    Hakuna mgomo kila kitu kinaenda kama ilivyopangwa!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2014

    Yaani hii nchi kila mtu ana mamlaka yake.

    Hao wenye daladala hawataki mabadiliko wanataka kufany vitu kivyao.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 02, 2014

    KWANINI WATU HAWAPENDI KUFUATA SHERIA. WAANDAMANE ILI IWEJE? HATUTAKI HUO UCHAFU WAO UNAOITWA BIASHARA....BIASHARA KILA MAHALI, JAMANI TUFANANE NA NCHI ZINGINE, HAO MNAOWAITA WAFANYABIASHARA SANA SANA WENGI WAO NI WAHUNI WASIO NA KAZI WANAOJIFICHAFICHA KWENYE MIGONGO YA WENGINE ILI WAWEZE KUFANYA UHALIFU MDOGO MDOGO WA KUCHOMOLEA WATU FEDHA NA KUWAIBIA POCHI.....HATUWATAKI MUONDOKEEEE!!!!!! NA HIZO BAJAJ NAO WAJIFUNZE USTAARABU IKIWEZEKANA WAONDOLEWE PIA HAKUNA WANACHOKIFANYA ZAIDI YA KUSABABISHA AJALI NA KUPOTEZA MAISHA YA WATANZANIA. SERIKALI, MKUU WA MKOA, WILAYA NA WENGINE WAONDOENI HAO KWENYE MIJI YETU ILI IWE MISAFI....KAMA KUNA MTU ANAJIITA MFANYA BIASHARA BASI AKATAFUTE DUKA LA KUPANGA, KAMA HAWEZI BASI AFANYE KAZI NYINGINE....TUTAFIKA TU, MSIJALI KUNYIMWA KURA WAKATI WA UCHAGUZI WATANZANIA WENGI HAWATAKI KUWAONA HAO MACHINGA WAKIZIBA PAVEMENTS ZA BARABARA KWA KISINGIZIO CHA BIASHARA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 02, 2014

    Kuanzia leo ukitaka kwenda mwenge toka posta lazima Uwe na 800!! maisha matamu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 02, 2014

    Daaaah nilikuwa sijui hiyo bongo mnayosema tambarale ndio imechoka hivyo? Maskini mungu tunusuru yaani hiyo picha hapa naona kama kiama ni kesho tu , Hivyo ndio watanzania wanavyoishi katika hali duni kiasi hicho yaani bado sana sana. Sasa hio ndi Dar mjini Capital city , Je huko vijijini ndio namna gani ? Shame on my country huo ndio usafiri wa mjini kweli?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mzee wazungu wanakufanya nini mpaka haupendi nchi yako hivyo!...lazima kuna kitu watakuwa wanakufurahisha nacho!!!

      Delete
    2. AnonymousJune 03, 2014

      Ninaishi Marekani katika moja ya majiji makubwa kabisa ya nchi hii. Lakini, bado naamini Tanzania ni nchi nzuri kuishi. Uzuri wa miji na huduma huku ughaibuni havikupatikana kwa ndoto za mchana bali kwa kufanyakazi. Wito wangu badala ya kulalamika turudi nyumbani tutumie exposure na uzoefu kuleta maendeleo badala ya kuponda nchi yako mwenyewe ilhali unawajibu wa kuitumikia

      Delete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...