Na Sultani Kipingo
wa Globu ya Jamii
Uwezo wa kifedha wa Nike unaipaisha kampuni
hiyo katika vita vya Kombe la Dunia 2014 kwa kuiongoza kampuni ya Adidas kwa mabao 4
katika awamu ya makundi ya michuano hiyo huko Brazil.
Kampuni ya Nike ambayo ndio kubwa zaidi
duniani kwa vifaa vya michezo imeonesha umwamba wake baada ya nyota
inayowadhamini kufunga mabao 61 katika awamu hiyo ya makundi, huku Adidas
ikifuatia kwa magoli 57.
Lakini Adidas wanaweza kupata ahueni kwa kuwa
na njumu bora, kwa mujibu wa wataalamu wa mambo hayo. Kiatu cha Adizero
kinachovaliwa na nyota wakali kama Lionel Messi, Robin van Persie, Arjen Robben,
Karim Benzema na Thomas Muller
kimechangua magoli 38 katika awamu hiyo, huku kiatu cha Nike cha Superfly IV
kinachovaliwa na
Alexis Sanchez wa Chile na Xherdan Shaqiri wa Uswisi kimepiga
mabao 21 hadi sasa (kabla mechi za mtoano kuanza).
Adidas pia wanaongoza katika chati ya magoli
ya kusaidia, kwa kuchangia mabao 65 katika awamu ya makundi, dhidi ya 54 ya
Adidas, wakati kampuni ya Umbro ikijikongoja kupata goli, na hadi sasa ina goli
moja la usaidizi kwa mchezaji Mauricio Pinilla aliyetoa pasi katika mchezo wa
Chile dhidi ya Australia, ila kiatu chao hakijafunga bao hadi sasa.
Wachezaji wanaovaa kiatu cha Puma wamefunga
mabao manane, wakati kampuni ya Mizuno na Warrior kila mmoja akichangia mabao
matatu. Kampuni ya Under Armour pia imemaliza awamu ya makundi bila kupata bao.
Nike wanaomdhamini Neymar wa Brazil wana mabao 61
Cristiano Ronaldo wa Ureno anadhaminiwa na Nike
Robin van Persie wa Uholanzi anavaa kiatu cha Adidas aina ya Adizero
Adidas wanaomdhamini Lionel Mesii wa Argentina wana mabao 57
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...