Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa pili kulia),
akipata maelezo juu ya Mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma kutoka kwa Meneja
Utawala Msaidizi wa kampuni ya Tanzania –
China International Mineral Resources Limited (TCIMRL) Bw. Israel Mkojera.
Pamoja nae ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NDC Bw. Mlingi E. Mkucha (wa kwanza
kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda Mama wa NDC Bw. Ramson Mwilangali (wa
kwanza kushoto), Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango Bi. Florence Mwanri (wa
pili kushoto), Erasmus Masumbuko, Tume ya Mipango (wa tatu Kushoto).
Viongozi
pamoja na Maofisa kutoka Tume ya Mipango wakiangalia sehemu ambayo makaa ya
mawe yanaonekana juu ya ardhi. Kulia ni mhandisi wa madini kutoka kampuni ya TCIMRL. Kampuni hii ni ya ubia kati ya
Serikali ya Tanzania, na kampuni ya Sichuang Hongda Group Limited ya China.
Sehemu
ambayo makaa ya mawe yanaoneka kwa juu katika uhalisia wake.
Shimo hili lilichimbwa
mwaka 1956 kwa ajili ya utafiti kuangalia tabaka za makaa ya mawe katika eneo
hilo la Mchuchuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...