Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa Qs Mhonda J Entertainment, Joseph Mhonda, amesema kwamba mwenye uwezo wa kupunguza makali ya mwimbaji Nassib Abdul Diamond ni Mbwana Mohamed ‘Mb Dog’ pekee.
Msanii Diamond, pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mhonda alisema hiyo inatokana na ubora wa wasanii hao, pamoja na aina yao inayovitia kuwasikiliza.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Qs Mhonda J Entertainment, Joseph Mhonda pichani.
Alisema Diamond ni msanii mkali ambaye kwa mtindo wake huenda akakosa mpinzani, kama Mb Dog atazidi kushuka thamani yake kisanaa.


Msanii Mb Dog, pichani.
“Kila nikimuangalia Diamond Napata shauku ya kuona makali ya Mb Dog yanarudi kwasababu ndio anayeweza kuleta ushindani kwa mwimbaji huyo anayetamba na mtindo wake wa Ngololo.

“Mb Dog ana ladha nzuri, sambamba na uimbaji wake unaovutia bila kusahau ubunifu pia katika tungo zake, hivyo kwa kiasi kikubwa yeye ndio mpinzani wa kweli wa Diamond na si mwingine,” alisema.

Mb Dog kwa sasa anatamba na wimbo wake Mbona Umenuna, akiimba kwa hisia kubwa, huku akiwa na shauku ya kurudi makali yake ya zamani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2014

    Afanye yake,kutwa mnajilinganisha na Diamond,tatizo letu twapenda kucopy&paste!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...