Afisa Viwango na Ubora wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, Ndeonasia Towo akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu salama inayoratibiwa na Diwani wa Chama cha Mapinduzi wa Kata ya Kipawa, Bonna Kaluwa (katikati) iliyozinduliwa katika Ukumbi wa Arnaotoglu na kilele chake kitakuwa Juni 22, mwaka huu kwenye viwanja vya Sitakishari Kata ya Kipawa, Dar es Salaam. Kampeni hiyo inalengo la kuchangisha damu ili kupunguza vifo vya wanawake wakati wa kujifungua kutokana na ukosefu wa damu.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa kampeni ya uchangishaji wa damu iliyozinduliwa Dar es Salaam leo na Diwani wa Kata ya Kipawa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bonna Kaluwa.
Diwani wa Kata ya Kipawa (CCM), Bonna Kaluwa ( wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Arnaotoglu, Dar es Salaam leo kuhusu uzinduzi wa kampeni yake ya kuchangisha damu salama ili kuokoa vifo vitokanavyo na ukosefu wa damu hasa vya uzazi. Kilele cha kampeni hiyo ni Juni 22, mwaka huu kwa maandamano yatakayoanzia katika viwanja vya Gonga Majumbasita hadi viwanja vya Sitakishari ambapo mgeni rasmi atakuwa Mstahiki Meya wa Ilala, Jerry Silaa.damu salama ili kuokoa vifo hivyo. Kampeni hiyo imezinduliwa Dar es Salaam leo na kilele chake ni Juni 22, mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...