REDIO tatu  zenye majina  na masafa marefu zimejitosa kutangaza shindano la Redd’s Miss Pwani 2014.
 
Akizungumza jana Mratibu wa shindano hilo  Khadija Kalili alisema kwamba amepata udhamini wa matangazo kutoka Redio 5,  Times FM  na Redio Clouds FM.
 
Kalili alisema kwamba  hivi sasa joto kwa warembo limepanda huku kila mmoja akiwa na ari ya kunyakua taji hilo siku  hiyo Juni 27.
 
Redd’s Miss Pwani imepangwa kufanyika Juni 27  mwaka huu kwenye ukumbi wa Maisha Plus (Police Mess).
 
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa bendi ya  muziki wa dansi ya  Extra Bongo inayoongozwa  na mwanamuziki mkongwe nchini Camarade Ally Choki  ndiyo itakayopamba shindano  hilo.
 
 
Mbali ya Choki ambaye atakuwa na kikosi chake kikali cha wacheza shoo kinachoongozwa na Mussa Hassan Nyamwela pamoja na wanenguaji wa kike kama Maria Soloma , Asha Said ‘Sharapova’ , Otilia na wakali wengine.
 
Shindano hilo  limeandaliwa na Kampuni ya Linda Media Solutions (LIMSO).
 
Alisema katika shindano hilo warembo 12 watapanda jukwaani ikiwa ni katika kumsaka malkia wa Mkoa wa  Pwani ambaye atakuwa mwakilishi katika  shindano la kanda ya Mashariki na baadaye katika fainali za Redd’s Miss Tanzania 2014 zitakazofanyika  baadaye mwaka huu.
 
Kalili aliwataja  wadhamini wa Miss Pwani ni Redd’s Premium Cold, DIRA Media Group,   Eden Herbalist Clinic ya Jijini Dar es Salaam, CXC Africa, Kitwe Traders, Michuzi Media Group, Jambo Concept Tanzania Limited, Bongoweekend.blogspot.com, Maisha Plus (Police Mess) ,  Montage, Filbert Bayi Foundation (FBF).
 
Kiingilio ni sh. 10,000.
 Hao pichani ni baadhi ya washiriki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...