Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Terezia Mmbando (kulia) akitoa taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU na Ukimwi katika jiji la Dar es salaam kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho alipotembelea maeneo mbalimbali ya jiji hilo kuangalia hatua zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo katika ziara yake ya siku nne.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akitoa tathmini ya hali ya maambukizi ya VVU katika jiji la Dar es salaam na hatua zinazochuliwa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kukabiliana na janga hilo mara baada ya kupokea ugeni kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi.
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa ambaye pia ni diwani wa kata ya Gongolamboto akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho kwa kuhusu hatua iliyofikiwa na mikakati ya manispaa ya Ilala katika kukabiliana na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na viongozi na wakazi wa kata ya Gongolamboto jijini Dar es salaam alipotembelea eneo hilo kuangalia hatua zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo katika ngazi ya kata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2014

    Ohhh!

    Tuacheni ngono zembe hali ya Ripoti hiyo inatisha TUTAKUFWAAAAA kwa kuwa Idadi ya Miji ya Makaburini (MAKABURI) itakuwa mikubwa na Makazi Mengi zaidi ya miji ya Maisha hai (NYUMBA ZA WALIOBAKI HAI).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...