Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mji mkuu wa Equatorial Guinea wa Malabo leo Juni 24, 2014 kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Africa –African Union (AU).
Akiwa Malabo, Mheshimiwa Rais Kikwete pia atakuwa Mwenyekiti wa kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa AU kitakachojadili mazingira. Rais Kikwete na ujumbe wake anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Equatorial Guinea Mhe Vicente Ehate Tomi alipowasili katika katika uwanja wa ndege wa Malabo, Equatorial Guinea, leo Juni 24, 2014
PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Malabo, Equatorial Guinea, leo Juni 24, 2014
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM.
JE NI LINI MKUTANO WA AFRICAN UNION UTAFANYIKA TANZANIA? MKUTANO ULISHAFANYIKA KENYA, UGANDA ,MALAWI. SIJASIKIA KWETU.....AU HATUNA HOTEL ZA KUTOSHA ZA KUWALAZA MARAIS WA AFRICA?
ReplyDelete...Swali zuri sana mdau wa 1.Natumaini tutapata majibu hapa hapa kama kuna utaratibu unaotumika.
ReplyDeleteSWALI KWA WATU WA DIPLOMASIA.Salaam za viongozi wanaotoka nchi zinazotofautiana kwa Lugha wanatumia lugha gani kusalimiana?Mfano hapo EQ Guinea(Spanish),Tanzania(Swahili/English).ENGLISH?
David V
Jibu ni Mkutano wa 29 wa AU mwaka 2017 [http://archive.dailynews.co.tz/index.php/local-news/7590-dar-to-host-au-summit-in-2017] Mimi binafsi naamini itafanyika Dar katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere [JNICC] na pia Dar ina hoteli mengi za kifahari.
ReplyDelete@David, ingawa mimi si mwanadiplomasia, nimewahi kumsikia JK akiongea Kifaransa na marais wa Benin na Madagascar. Nimemsikia akitamka neno "bienvenu". Pia, nakumbuka kumsikia rais wetu akiongea Kichina wakati wa ziara wa Rais Xi Jingpin na waandishi wa habari - nili bookmark ile link lakini mpaka sijafanikiwa kuitafuta.
https://www.youtube.com/watch?v=gP0T_efyubA&t=0m50s [JK na Rais wa Madagascar]
https://www.youtube.com/watch?v=FkJrBD5xHbg&t=0m30s [JK na Rais wa Benin]
Lugha siyo tatizo kuanzia mikutani ya kimataifa hadi kombe la dunia. Teknolojia imemaliza hilo tatizo. Tatizo kwa Tanzania ni foleni na barabara kujaa maji na kugeuka mito baada ya mvua ya dakika tano.
ReplyDeleteWadau mwacheni Jakaya Kikwete aitwe Dakitari!
ReplyDeleteKama anavyosema Mdau wa 3 Ndugu Ali kumbe Raisi wetu anazo Lugha nyingi kichwani?, anajua Kifaransa, Kichina na Lugha zingine sio?