Na Greyson Mwase, Tarime
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia madini Stephen Masele amekemea vikali tabia ya wamiliki wa migodi kuajiri watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 kwani inarudisha maendeleo ya watoto hao na kwa jamii kwa ujumla inayowategemea
Waziri Masele ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa semina iliyoshirikisha wachimbaji wadogo, madiwani, viongozi wa vijiji, wilaya, madiwani pamoja na viongozi wa vyama vya siasa inayoendelea katika jimbo la Mwibara wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Waziri Masele alisema kuwa kumekuwepo na tabia ya wamiliki wa migodi, ikiwa ni pamoja na wazazi wenye watoto wenye umri chini ya miaka 18 kuruhusu watoto hao kufanya kazi kwenye migodi badala ya kuwahimiza kwenda shule na kupata elimu itakayowasaidia kutoka kwenye giza.
wazazi wawajibike watoto waende shule siyo kutafuta pesa za kujikimu wakiwa wadogo.
ReplyDeleteInapiga marufuku lakini utekelezaji utakuwaje?
ReplyDelete