TAMPRO inayofuraha kwa heshima na taadhima kukuarifu kufanyika kwa Kungamano la Sita la Kukaribisha Mwezi wa Ramadhan 1435H, Siku ya Jumapili Juni 22, 2014 Katika ukumbi wa Julias Nyerere International Convention Centre (JNICC) – Shaaban Robert Street,Dar es Salaam kuanzia saa 02:30 Asubuhi Mpaka Saa 10:30 Alasiri.

TAMPRO ni Taasisi ya wanataaluma wa Kiislamu katika fani mbali mbali iliyosajiriwa Mwaka 1997 kwa lengo la kuwaleta pamoja wanataaluma wa kiislamu kulitumikia taifa huku wakiendelea kuimarisha misingi na thamani za matendo bora ya kiislamu.

Wanachama wake hutokea katika taaluma mbali mbali zikiwemo za Afya, Uchumi, Uhandisi, Elimu, Sheria, Usimamizi wa Biashara pamoja na nyanja mbali mbali za Uongozi na sayansi za jamii.
Kwa Miaka Sita Mfululizo, TAMPRO imejenga utamaduni wa kuwaalika Waislam Mbali mbali kujumuika pamoja katika Jumapili ya Mwisho ya Mwezi wa Shaaban katika kongamano la kuwaandaa na kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan “Welcoming Ramadhan Conference” ili kufahamiana, kudumisha udugu, Kuwa Karibu na Wanazuoni wa Kiislam na kuonyesha uwepo wao katika Jamii.
Katika Kongamano la Mwaka huu “The 6th Welcoming Ramadhan Conference 1434H” Anwani ya Mkutano itakuwa ni “Vijana Wetu, Hazina Yetu” ambapo mambo kadhaa yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na Mafanikio na changamoto zinazowakabili Vijana katika jamii.

1. Sheikh, Mwanasayansi, Profesa Mohammed Badamana kutoka Chuo Kikuu Cha Nairobi atazungumza kuhusu “Changamoto za kuwalea vijana wa kiislam katika dunia ya sasa inayobadilika kwa haraka”
2. Sheikh Mh. Amir Mussa Kundecha, Kutoka Baraka Kuu la Jumuia na Taasisi za Kiislam ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba atazungumza kuhusu “Qur an Tukufu, Katiba mpya ya nchi yetu na Mustakbali wa Vijana wa Kiislam”
3. Ndugu Ali Masoud Maarufu Kama Masoud Kipanya atazungumza kuhusu “Vijana, Vyombo vya Habari na Utandawazi”
Karibu Ujumuike na Waislamu Wanaataluma mbali mbali zaidi ya 600katika kusukuma mbele Uislamu kwa kujuana na kuongeza Mshikamano wa Wanazuoni Wetu Mbali Mbali. Mchango wa ushiriki na Maandalizi ya Kongamano ni TZS 30,000 kwa Mtu na TZS 50,000 kwa Mke na Mume. Mume mwenye Mke Zaidi ya Mmoja atapewa upendeleo Maalum.
Tuna matumaini makubwa na kupata uwakilishi wako katika shughuli hii pamoja na kuwafikishia taarifa hii wanataaluma wengine watakaoweza kufika na kujumuika Pamoja.

Kadi za Ushiriki zinapatikana Ofisi za TAMPRO Makao Makuu Magomeni Usalama karibu na Ofisi za Manispaa ya Kinondoni, Dar es salaam au Piga Simu namba hizi ili kuletewa au kuwekewa kadi yako:0688 130828.   0714151532 .   0767 151532
In sha Allah Mwenyezi Mungu atufikishe salama na atufanyie wepesi kujumuika na kutimiza malengo ya mjumuiko huu.

Maassalaam

Mohamed,
Mwenyekiti, Kamati ya Maandalizi
+255787670714 or 0767565560.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2014

    Ahsante kwa taarifa, Allah atujaaliye tuwe miongoni tutakaoifunga ramadhani inayokuja na atujaaliye mwisho mwema

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2014

    JazaakaALLAH khayr....

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2014

    Amin Thuma Aaaamin

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 28, 2014

    Mizimu ya mababu zetu iwalinde ili jitihada hizi ziendelee kulinda amani katika nchi yetu tukufu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...