Assalaamu Alaykum
Wa Rahmatul Lah
Inshaa Allah
Jumapili tarehe 22 Juni 2014 itakuwa ndiyo siku ya Ufunguzi Rasmi wa Jengo la Kituo
cha An Noor Leicester (An Noor Community Centre) pamoja na Masjid An Noor
Maimamu wa
Misikiti yote ya mjini Leicester wamealikwa kuhudhuria katika mjumuiko Maalumu
ambao utakuwa na lengo la kutambuana rasmi, kuimarisha Ushirikiano na kufungua
milango kuwakaribisha rasmi Maimamu wa Leicester na Wafuasi wao
Wanakamati wote wa
Jumuia ya An Noor pia watahudhuria katika mjumuiko huu ambao Inshaa Allah
unatarajiwa kuwa wa aina yake
Maimamu teule
watapewa fursa ya kutoa Mawaidha, na kabla ya hapo Uongozi wa Masjid utasoma
Risala ya Jumuia, ambayo itatoa picha kwa Muhtasari ya maendeleo ya An Noor
Community Leicester.
Kituo
kimekwishaanza kutumika toka Mwezi wa Juni 2013
UTARATIBU wa Siku ya
Ufunguzi ni huu ufuatao:
SIKU: Jumapili 22 Juni 2014 Saa Kumi Mpaka Saa kumi na
Mbili Kamili Jioni (4pm-6pm)
WAALIKWA: - Maimamu wa Misikiti Leicester na Wanakamati
Wote wa Jumuia ya An Noor
PAHALA: 170a Belgrave Gate, Leicester, LE1 3XL
Kwa Maelezo tafadhali
wasiliana na Sheikh Abdul Dau, Katibu wa Kamati ya Shura 07913905527
Wa Billahi
Tawfeeq
kila la kheri
ReplyDeleteMasha Allah. Hongera An Noor!
ReplyDeleteMwenyezi Mungu akupeni nguvu zaidi na zaidi ya kulisimamisha jina lake hata nje ya mipaka ya mlikotoka. Amin.
Mndengereko Ukerewe
Kwa mara nyingine tena jina "Dau" linaendelea kung'ara katika mambo ya kheri. Hongera sana familia ya Dau. Allah amekuchagueni na mmekubali kuchaguliwa. Mmekuwa mstari wa mbele hapa duniani, twamuomba Allah akupeni mafanikio zaidi hapa ulimwenguni na akuwekeni mstari wa mbele huko Akhera. Amin
Alhamdullilah mwenyezimungu atujaalie umoja na mshikamano.
ReplyDelete