Assalaamu Alaykum Wa Rahmatul Lah
Inshaa Allah Jumapili tarehe 22 Juni 2014 itakuwa ndiyo siku ya Ufunguzi Rasmi wa Jengo la Kituo cha An Noor Leicester (An Noor Community Centre) pamoja na Masjid An Noor
Maimamu wa Misikiti yote ya mjini Leicester wamealikwa kuhudhuria katika mjumuiko Maalumu ambao utakuwa na lengo la kutambuana rasmi, kuimarisha Ushirikiano na kufungua milango kuwakaribisha rasmi Maimamu wa Leicester na Wafuasi wao
Wanakamati wote wa Jumuia ya An Noor pia watahudhuria katika mjumuiko huu ambao Inshaa Allah unatarajiwa kuwa wa aina yake
Maimamu teule watapewa fursa ya kutoa Mawaidha, na kabla ya hapo Uongozi wa Masjid utasoma Risala ya Jumuia, ambayo itatoa picha kwa Muhtasari ya maendeleo ya An Noor Community Leicester.
Kituo kimekwishaanza kutumika toka Mwezi wa Juni 2013
UTARATIBU wa Siku ya Ufunguzi ni huu ufuatao:
SIKU:                     Jumapili 22 Juni 2014 Saa Kumi Mpaka Saa kumi na Mbili Kamili Jioni (4pm-6pm)
WAALIKWA:      - Maimamu wa Misikiti Leicester na Wanakamati Wote wa Jumuia ya An Noor
PAHALA:              170a Belgrave Gate, Leicester, LE1 3XL
Kwa Maelezo tafadhali wasiliana na Sheikh Abdul Dau, Katibu wa Kamati ya Shura 07913905527
Wa Billahi Tawfeeq

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 15, 2014

    kila la kheri

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 15, 2014

    Masha Allah. Hongera An Noor!
    Mwenyezi Mungu akupeni nguvu zaidi na zaidi ya kulisimamisha jina lake hata nje ya mipaka ya mlikotoka. Amin.
    Mndengereko Ukerewe
    Kwa mara nyingine tena jina "Dau" linaendelea kung'ara katika mambo ya kheri. Hongera sana familia ya Dau. Allah amekuchagueni na mmekubali kuchaguliwa. Mmekuwa mstari wa mbele hapa duniani, twamuomba Allah akupeni mafanikio zaidi hapa ulimwenguni na akuwekeni mstari wa mbele huko Akhera. Amin

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 15, 2014

    Alhamdullilah mwenyezimungu atujaalie umoja na mshikamano.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...