Mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mhe Juma Abeid akifuatilia sherehe hizo katika viwanja vya Shule ya Msingi Kiparang’ada. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Kiparang’anda Mhe Karu Amani Karavina, na Kulia ni Mke wa Mbunge wa Mkuranga,Mama Naima Malima.
Mke wa Mbunge wa Mkuranga,Mama Naima Malima akizungumza machache wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika,yaliyofanyika Juni 16 katika shule ya msingi Kiparang'anda,wilayani Mkuranga.Kushoto ni Mgeni Rasmi katika sherehe hizo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mhe Juma Abeid
Mke wa Mbunge wa Mkuranga,Mama Naima Malima akikabidhi Sare na Vifaa vya shule kwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mhe Juma Abeid kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kiparang'anda,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku Mtoto wa Afrika.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mhe Juma Abeid akijaribu kusukuma Baiskeli ya walemavu iliyotolewa na Mke wa Mbunge wa Mkuranga ajili ya watoto wenye uhitaji wa vifaa hivyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...