JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA TOFAUTI.
KATIKA MSAKO WA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EDGAR PATRICK (24) MKAZI WA MAPOROMOKO
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KILO 12 AMBAYO ALIIFICHA KATIKA NDOO YA
PLASTIC.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.06.2014 MAJIRA YA SAA 13:36 MCHANA KATIKA MTAA WA
MAPOROMOKO, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
MSAKO WA PILI:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JACKSON EMANUEL (22) MKAZI WA ILEMI
JIJINI MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA NOTI BANDIA
17 ZA TSHS 10,000/= SAWA NA TSHS 170,000/= NOTI 12 ZA TSHS 5,000/= SAWA NA TSHS
60,000/=.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.06.2014 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU KATIKA MTAA WA MAGEGE-ILEMI,
KATA YA ILEMI, TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. NOTI HIZO ZILIKUWA NA
NAMBA DW 5621984 – NOTI 17 NA NOTI 12 ZA TSHS 5,000/= ZIKIWA NA NAMBA BB
119382.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI
WATUHUMIWA ZINAENDELEA KUFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA ZAO. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUWA MAKINI
MATAPELI HASA KATIKA MAENEO YA BIASHARA PIA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WATU
WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA UTENGENEZAJI NA USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...