
Niwaombee salaam Wadogo zangu waliotekwa Nigeria, na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi kama vita.Kwangu ni dua kipindi hiki ili kuweka wepesi katika kuwatoa katika dhiki hizo kubwa.
Pia nitumie nafasi hii kuuambia Umma wa Tanzania na hasa wale watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wameendelea kuwa waathirika wa matumizi mabaya ya mitandao kuwa Hii ndiyo Account rasmi ya Ridhiwani Kikwete.Hizo account zingine ikiwemo
Ridhiwani J. Kikwete
Ridhiwani Kikwete official fan page
Ridhiwani Kikwete birth date 1983
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Ridhiwani Kikwete -nimevaa shati la Ccm
Na nyenginezo si account zangu,ni za watu ambao wamejisikia kutumia jina langu kwa sababu mbalimbali jambo ambalo nimeona katika siku hii ya leo nilikanushe. Kwa kauli ya kukanisha namaanisha kuwa hizi account sina mahusiano nazo kabisa na hawa wanaotumia Jina langu nawaomba waache mara moja kwani si jambo jema kuoongopea ummma wa Watanzania ambao wamekaa mitandaoni wakiamini wanafanya mawasiliano nami wakati kihalisia si mimi.
Mwisho, napenda kuwaambia Watanzania na wana mtandao wenangu kuwa haya Makundi yaliyoanzishwa kwenye mtandao kama
-YOUTH BATTLE
-VIJANA WANAOIPENDA NCHI YAO KWA MOYO
-SACCOS INAYOTOA MIKOPO
-UNGANISHAJI BODI YA MIKOPO etc.
Na mengineyo ni makundi ambayo sijawahi na wala sijashiriki kuyaasisi mimi.Ni hao ambao hawana nia njema na jina langu na heshima ya familia ambayo nimekuwa nahangaika kuihifadhi.
Account yangu halisi ni
RIDHIWANI KIKWETE ambayo kwenye profile picha yangu yuko bwana Reginald Mengi na Juzi nilitoa tangazo kukanusha habari za msiba wa Ndg.Shukuru Jumanne Kawambwa(Mb) wa Bagamoyo.
Hivyo naomba kutoa angalia kwa Watanzania wenzangu.
Nawaomba kuwasilisha.
Mimi
RIDHIWANI KIKWETE.
Naomba nikutie moyo ndugu yangu yote unayopitia ikiwemo kupewa kila kitu cha ufahali kwamba ni mali zako na mashambulizi mengine, hayo yote yanakuandaa na kukukomaza kuwa mwanasiasa na Kiongozi shupavu. Keep it up and don lose heart. Its me Bishop
ReplyDeleteNINGEOMBA VITAMBULISHO VYA URAIYA VILIPIWE ANGALAU GHARAMA KIDOGO KANI WATANZANIA HAWAJAJUWA UMUHIMU WA ID. WENGI WETU WANAVIACHA KWENYE MADUKA YA PHOTO COPY KWA GHARAMA YA Tsh 200/= HASWA WANAPO KOSA CHENJI YA KULIPIA COPY ZAO WANAVIWEKA REHANI NA HAWARUDI KUVIKOMBOWA NIMEKUTA VITAMBULISHA VYA WAPIGA KURA ZAIDI YA SABA VIMEBANDIKWA KWENYE DIRISHA LA DUKA MOJAWAPO MJINI BIHARAMULO OFISI YA COPY KWA MR KHATRY NA KWENGINEKO MWANZA BUKOBA KAHAMA. KAMA HAMNIAMINI PITIENI KWENYE MADUKA YA PHOTO COPY NCHI NZIMA UTAKUTA HALI NDIO HIYOOOO
ReplyDelete