Ndugu Fredricky Kajiru Mroki wa Kipera-Kinyenze Morogoro, anasikitika kutangaza kifo cha mtoto wake Eliewaha Kajiru (Pichani) kilichotokea alfajiri ya leo Nyumbani kwakwe Kipera. 

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Bibi yake Kinyenze, Mvomero Morogoro. Habari ziwafikie, Baba Mkubwa wa Marehemu, Lloyd Atenaka wa Kibaha Block B, Baba wadogo wa Marehemu, Dossa Mroki, Onesmo Nathan, Thomas Nathan, Daniel Nathan, Kyase Nathan na Mroki Mroki. Shangazi wa Marehemu, Stella Kaluse na Namche Mroki wa Dar es Salaam. Pia habari ziwafikie Babu wa Marehemu Agustino Shogholo Mgonja wa Pugu Kajiungeni na ukoo wote wa Kajiru, Mroki, na Shogholo popote pale walipo. 

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2014

    Mungu amrehemu huyu mtoto. Hii picha inasikitisha sana. Poleni wafiwa.

    ReplyDelete
  2. MOLA mlaze pema huyu Malaika wako aliyekwishafika kwako. Naungana na mdau wa mwanzo hapo juu, kweli hata mie hii picha imenitia huruma inasikitisha sana, maskini sijuwi alikuwa akililia nini au amechukizwa na nini. Pumzika kwa amani palipo pema peponi mpendwa mtoto wetu Eliewaha Kajiru. AMEEN.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...