Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiongea wakati wa mkutano wa Mawaziri wanaohusika na masuala ya Nishati ambapo aliwatangazia wajumbe hao kwamba Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Bara la Afrika kuhusu Nishati Endelevu katika muda utaopangwa na Umoja wa Mataifa.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa siku tatu wa Nishati Endelevu kwa Wote ( SE4ALL) ulioandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Eng. Yahya Samamba Katibu wa Waziri na Eng. Styden Rwebangila
Watanzania wengine ambao ni sehumu ya Ujumbe wa Tanzania. Kutoka kushoto ni Bi. Venosa Ngow ( TPDC) Eng. Leonard Masanja kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Eng Jones fredrick Olutu kutoka Wakala wa Nishati Vijijini ( REA)
---------------------------------
Na Mwandishi Maalum, New
York
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania imeelezea
utayari wake wa kuwa mwenyeji wa mkutano
wa Bara la Afrika kuhushu Nishati Endelevu kwa wote.
Ahadi
hiyo imetolewa siku ya Ijumaa, na Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter
Muhongo ( Mb) mwishoni wa mkutano wa
siku tatu , uliojadili kwa kina upatikanaji wa nishati endelevu kwa wote.
Mkutano huu uliojumuisha wadau wa kada
mbalimbali uliandaliwa na katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, ambapo pia palifanyika
uzinduzi wa mwongo wa nishati endelevu kwa
wote unaoanza 2014 hadi 2024.
“ Ninapenda kutaarifu kwamba, nimezungumza na Rais wangu, Tanzania iko tayari kuwa mwenyejiji
wa mkutano wa nchi za Afrika kuhusu
nishati endelevu. Tutakuwa wenyeji wa
mkutano huo pale Umoja wa Mataifa utakapokuwa tayari”. akasema Waziri Muhongo. Kauli iliyopokelewa vema na
waandaji wa mkutano huo.
Waziri
Muhongo ambaye ameshiriki kikamilifu
mijadala mbalimbali tangu mwanzo wa mkutano hadi mwisho, alisema Tanzania na
kama ilivyo kwa nchi nyingine nyingi
hasa za Afrika, Nishati Endelevu ni
muhimu katika utekelezaji na
ufanikishaji wa Maendeleo Endelevu
badaa ya mwaka 2015.
Akasisitiza
kuwa katika utekelezaji wa mpango wa
nishati mbadala kwa wote, Afrika
inapashwa kupewa kipaumbele cha pekee.
Katika
siku hii ya tatu na ya mwisho ya mkutano huu,
Mawaziri walioziwakilisha nchi zao, walipata fursa ya kubadilishana
mawazo, kuelezea uzoefu wao, kutoa maoni yao na halikadhalika kupendekeza nini cha kufanya ili hatimaye watu wengi zaidi
hususani katika nchi zinazoendelea
waweze kupata huduma hii ya nishati endelevu.
Inakadiriwa
kwamba zaidi ya watu 1.3 bilioni duniani kote hawana huduma
ya umeme na zaidi wa 2.6 bilioni wanatumia nishati asilia kwa kupikia na
kupata joto. Matumizi ya nishati
asilia yanasababisha watu 4.3 milioni kufariki kila mwaka kabla ya wakati wao
huku wengi kati yao wakiwa ni wanawake na watoto kutokana na uvutaji wa moshi.
Waziri
Muhongo ambaye ameongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu akiwamo
Muhandisi kutoka Wakala wa
Nishati Vijijini. Amesisitiza pia uhusiamo kati ya nishati na elimu kwa
kile alichosema ili mwanafunzi aweze kujiandaa au kujisomea vizuri anahitaji
nishati ambayo ni endelevu na yenye
uhakikia.
“ Hii itakuwa mara yangu ya nne kutoa maoni na mchango wangu na kwa sababu hiyo nisingepeda kutumia muda mwingi na
pengine kurudia kile ambacho
nimeshakisema huko nyuma. Nisisitize kwamba tunapozungumzia mpango wa nishati endelevu kwa wote basin chi za
afrika zinatakuwa kupewa kipaumbele cha
pekee, vile vile suala
la uwepo wa nishati endelevu lina uhusiano mkubwa na utekelezaji wa
maendeleo endelevu baada ya 2015.
Akasisitiza
kuwa Tanzania imejipanga vema katika
kuhakikisha kwamba wananchi wake
wanapatiwa huduma hiyo muhimu kwa
maendeleo yao na nchi kwa ujumla.
Akinukuu
wanafalsafa mbalimbali, Waziri Muhongo
amebainisha kwamba dhana hiyo ya
kumpatia huduma ya nishati endelevu kila mtu inawezekana ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake
pamoja na ushirikiano.
Baadhi
ya wazungumzaji katika mkutano huo wa
Mawaziri walieleza kwamba
inawezekana kabisa kutumia mifano
ya huduma za usambazaji wa simu za mkononi huduma ambayo imewafikia
watu wengi ikatumika katika usambazaji wa
nishati endelevu.
Wengine
walisisitiza umuhimu wa nishati mbadala kama vile wa matumizi ya nguvu za jua
na upepo kama moja wa eneo muhimu la
kuwafikia watu wengi. Huku baadhi wakisisitiza
umuhimu wakuwatumia wataalamu waliopo pamoja na tafiti ambazo zimekwisha
kufanyika kuhusu suala zima la nishati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...