WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kwanza katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuingia kwenye ubia na sekta binafsi katika mradi mkubwa wa usafirishaji abiria.
Ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano yenye lengo la kuutangaza mradi wa mabasi yaendayo kasi kwenye ukumbi wa Mlimani City. Mkutano huo wa siku mbili, utamalizika kesho.
Waziri Mkuu amesema kutèkelezwa kwa mradi huo kutatoa fursa za ubunifu utakaowezesha kupatikana kwa suluhisho la usafiri mijini na hasa kwenye miji ambayo inakua kwa kasi barani Afrika.
"Mbali ya kutoa huduma za hali ya juu, za haraka na ambazo siyo ghali kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, nia ya Serikali ni kuona mfumo mpya wa matumizi ya kadi kwenye mpango huu wa usafiri unatumika ipasavyo," alisema.
Alisema ni matumaini ya Serikali kwamba wadau kutoka sekta binafsi ambao ni wazawa na wa kutoka nje ya nchi watashiriki kwenye mradi huu ili uweze kuboresha matumizi ya kadi ambayo mtu hatatakiwa kulipia fedha taslimu akiwa ndani ya basi bali kutumia kadi anayoilipia kabla ya kuingia ndani ya basi husika.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Serikali iliamua kuanzisha mradi huo ili kupunguza msongamano wa magari kwenye barabara za Jiji la Dar es Salaam.
"Hii ni awamu ya kwanza ambayo inakaribia kukamilika na inaanzia Kimara hadi Kivukoni na itakuwa na matawi mawili ya Morocco na Karikoo. Mradi wote una awamu sita za ujenzi kuelekea maeneo tofauti ya Jiji," alisema.
Mbali na mradi huo wa mabasi yaendayo kasi, Serikali inaangalia uwezekano wa kutumia usafiri wa majini kwa kutumia boti kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.
“Vilevile tutaimarisha usafiri wa reli kama njia nyingie ya kupunguza tatizo hili. Dk. Mwakyembe (Waziri wa Uchukuzi) ameanza na sote tumeona ni jambo linalowezekana. Cha msingi ni kuimarisha tu usafiri huu,” aliongeza Waziri Mkuu.
Mapema, akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia alisema Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa.
Pia alitumia fursa hiyo kuishukuru Benki ya Dunia ambayo alisema imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya kufadhili mradi huo.
Mkutano huo unawashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wa ndani na wa nje wanaotarajiwa kutoa huduma za mabasi makubwa na madogo, utoaji tiketi, ulinzi, usafi na huduma za maduka.
Waziri Mkuu, izengo Pinda akifungua Mkurano wa Majadiliano wa Kutangaza Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (Dar Rapid Transit) kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, leo Juni 3, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Majadiliano wa Kutangaza Mradi wa Mabasi yaendayo haraka kwenye ukumbi wa Mlimani City jijiniDar es salaam Juni 3, 2014. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Hawa Ghasia
Waziri Mkuu,, Mizengo Pinda akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Philippe Dongier baada ya kufungua Mkutano waMajadiliano wa kutangaza Mradi wa Mabasi yaendayo haraka kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Juni 3, 3014.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
...kasi maana yake nini? Kilometa ngapi kwa saa? Au jina ndilo lenye kupotosha? Mi ninachojua ni mabasi yenye njia maalum, ambako magari mengine hayapiti (na hapa nasubiri kwa hamu kubwa kuona kama madreva wetu wa Bongo wenye haraka kama wataheshimu hizo njia!), welcome civilization in TZ!
ReplyDeleteHongera sana Tanzania na Serikali. Kasoro moja. Jiji la DAR ES SALAAM lina barabara nyingi zisizo na alama za barabarani, mwendo kasi, halina taa za barabarani, uchofu unatupwa barabarani kwa kukosa sehemu maalum za kutupa uchafu huo. Je barabara hizi zitadumu kweli? Maana mitalo yote itajazwa uchafu kama ilivyo kariakoo. Hii ni aibu.
ReplyDeleteNi kweli uchafu Dar unatisha mitaa yote ya kariakoo uchafu unawekwa barabarani. Kama Jiji haliweki makontena ya kutupia uchafu linategemea nini? Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Mabalozi, Wakuu wa vyma vya siasa, wabunge, mameya, wakuu wa wilaya, na kila aina ya viongozi wote wanaishi Dar. Lakini ukizunguka huwezi kuona hata kontena moja la kutupia uchafu. Sasa kama hawa wote wanaishi Dar na haya hawayaoni...unategemea nini! Labda malaika ashuke.
ReplyDeletenina wasiwasi mapipa ya uchafu yakiwekwa yataibiwa au hayatatumika ipasavyo. Labda watu waelimishwe matumizi na magari special yakukusanya yaandaliwe. Huu utakuwa tena mradi upya ambao utawezesha watu kujipatia ajira
ReplyDeleteMimi wasiwasi wangu ni ajali za barabarani hasa wale waendao kwa miguu. Tumejizoelea kuvuka tu barabara kwa sababu hakuna heshima kwneye Zebra crossing sasa wakiweka na haya mabasi ya kwenda kasi si watoto watakwisha? Elimu inatolewa katika hili?
ReplyDeleteMimi swali langu ni juu ya matumizi ya lugha iliyozoeleka: bank ya dunia imetoa million Mia mbili za ufadhili! Je siyo Mkopo tunaotakiwa kulipa back na riba juu? Na tutaurejesha lini?
ReplyDeletenadhani elimu ya usalama barabarani ikitolewa ilenge hasa mashuleni kama kipindi kama wanavyofanya wenzetu ktk nchi zilizoendelea. pia alama za barabarani ziwekwe na watu wote waelimishwe na kuhamasiswa kuziheshimu. pia watumoaji barabara waache kudharau sheria sio za barabarani tu hata sheria zote za nchi waache ile ya kusema nina kizito serikalini au watautmia hela zao kudhoofisha sheria kwa kuhonga ili wasiadhibiwe kwa kuvunja sheria
ReplyDeletenadhani watu wakianza kufikiria sana usalama na kuhisi watavukaje basi maendeleo hayataletwa basi watu tunatakiwa tubadilike na kuenda na wakati. tumeshaambiwa yataaenda kasi basi na tuwe makini tutumie vivuko kwa usahihi pale tunapoambiwa tutumie alama za punamilia tuzitumie na madereva waziheshimu na kuzngatiea sheria za usalama barabarani.
ReplyDelete