Katika wiki chache zilizopita kulikuwa na msuguano kati ya serikali ya Marekani na China. Serikali ya Marekani inailaumu China kwa kufanya udukuzi kwenye kampuni zake na biashara nyingine, wakati China nayo ikiilaumu Marekani taarifa juu ya hili (inaweza kusomeka "HAPA" ).
Uchina baada ya hali hiyo ikaamua kukataza matumizi ya windows 8 kwenye kompyuta zote za serikali na taasisi zote zinazopewa fedha na serikali ya nchi hiyo na hili linaweza kusomeka kwa kirefu na viambatanishi vingine "HAPA"
Serikali ya China na wataalamu wake kadhaa wanasema matumizi ya windows 8 ni hatari kwa usalama wao na ustawi wao, hivyo wamekataza na kuendelea kutengeneza program yao ya COS China Operating System kwa ajili ya matumizi ya serikali pamoja na taasisi zake .

Kwa nchi za Ulaya suala kama hili liliwahi kutokea miaka kadhaa iliyopita , lakini Umoja wa Ulaya ulienda mahakamani na mahakama ikaamua Microsoft itoe source code kwa Umoja wa Ulaya ili waweze kubadilisha na kuweka mambo yao kwa maslahi ya umoja wa ulaya .
Kitu kikubwa ambacho serikali ya Uchina inalalamikia kuhusu Windows 8 ni hii source code, ambapo inataka source code ya bidhaa hii ili iweze kuifanyia mabadiliko iendane na maslahi yake haswa kwenye mambo ya ulinzi na usalama.
Hapa nchini kwetu tumeona taasisi mbalimbali na wizara mbalimbali za serikali tena nyeti zikitumia bidhaa mbalimbali za windows bila kufanya mabadiliko yoyote kwa ajili ya usalama wao. Tumeona watu haswa viongozi wakinunua kompyuta na vifaa vingine vya mawasilino na kuvitumia kuhifadhi taarifa nyeti bila vifaa hivi kuchunguzwa au kubadilishwa chochote.
Suala la serikali ya China lituamshe na tuanze harakati za kuangalia maslahi makubwa ya taifa wakati wa manunuzi na matumizi ya vifaa na program mbalimbali toka nchi za nje, maana program hizi na vifaa vyake vinaweza kutumika kwa urahisi kuhamisha taarifa na chochote kile au kufanya uhalifu bila mnunuzi au mtumiaji kujua.
Wakati serikali inafikiria kupeleka muswada wa sheria ya usalama wa mtandao bungeni, ni vizuri pia suala kama hili lijulikane mapema na wataalamu watakaojadili sera au chochote kinachohusiana na usalama wa Taifa .
Huwezi kulinda taifa kama taarifa zako zinaweza kuchukuliwa au kuangaliwa na mtu akiwa popote duniani. - kupata chanzo BOFYA HAPA
Nakubaliana sana na habari hii. Tanzania inabidi tuache kufanya kazi kwa mazoea. Ningetegemea leo hii tuwe mbali kuamasisha matumizi ya open source kuliko hizi za Microsoft lakini wapi.
ReplyDeleteTunafanya mambo yetu kuwa siri wakati dunia ya leo siyo hivyo. Tunatakiwa kwendana na dunia ya leo, tuache mambo ya miaka ya nyuma.
Mdau,
shuleni
Kulikuwa na protest campaign kupinga matumizi ya Microsoft's Window 8 kwenye vyuo vikuu vya Marekani mwezi uliopita! soma hapa baadhi ya sababu
ReplyDeletehttp://www.gnu.org/philosophy/malware-microsoft.html
Kwa kifupi, kuna haja kubwa ya kuufahamisha umma kwa ujumla na kuwahamasisha matumizi ya program huria na kwenda mbali zaidi kwa kuwahasisha kujilinda na matumizi ya mtandao
Tanzania Operating System (TOS) iko tayari? China wana jeuri ya kupambana na ma-giant ya dunia kama Microsoft kwa sababu waliwekeza kwenye elimu sana kiasi kwamba wana 'pool' ya wataalamu wa kuweza kutengeneza kitu wanachokitaka. Siku za nyuma tulizembea sana kwa kuwasomesha na kuwapatia elimu bora vijana wetu! Leo hii dalili hazioneshi kama tumebadilika! Mambo wanayoongelea bungeni sioni kama wameshashtuka kwamba elimu imepoteza mwelekeo!
ReplyDeleteKwa ufupi, tumepoteza visheni, ndio maana takribani kila mtanzania anataka "short-cut": mwanafunzi anaiba mtihani, mwingine anagushi cheti, mwenye elimu kazini anataka aibe, baadhi ya wanasiasa wanakuwa mafisadi, mfanyabiashara hataki kuzalisha anaona bora kuchuuza, mihadarati na pembe za ndovu, viungo vya albino imekuwa "dili" n.k.
Kwa ufupi, we are more vulnerable than ever with respect to our national security because we are vulnerable at an individual level!
Unajua wa-TZ hawako na motisha ya maisha yao kuanzia elimu wanayoipata na maisha ya kila siku wanayoishi! Ni vizuri semina kama hii mnayotangaza kwenye hii Blog (Brian Tracy na mwenzake) isaidie kuamsha ari ya wa-TZ wajue kuwa kuna maisha mazuri bila short-cut! Semina kama hizo ni nyingi sana kwa wenzetu, na attendance inazidi hata kwenye baadhi ya makanisa! Majina kama Les Brown, Tony Robinns, Jim Rohn (marehemu), Steven Covey (marehemu), Zig Ziglar (marehemu), Robin Sharma, Susan Jeffers, Earl Natinghale (marehemu), n.k. ni wengi mno, na wote wana kazi moja tu: kuamsha ari ya binadamu ifanye kazi kwa uwezo wake wote! Ni swala la kukumbushana, wala sio kulaumiana!!
Bila hilo, tutaishia kwenye udhoofu uliokithiri na kutawaliwa na mataifa yanayofuata visheni zao!
Mkuu asante sana kutukumbusha. Umbumbu nao unatusumbua ndio maana vitu kama hivyo hatuvifanyi.
ReplyDeleteUmbumbu Umbumbu Umbumbu Umbumbu Umbumbu ndio tatizo la TZ.
ReplyDeleteNapenda kuendeleza maoni kwa kutoa ushauri wa kua swala la kujiweka salama dhidi ya uhalifu mtandao lina fanana kabisa na swala la kujiweka salama dhidi ya uhalifu wa kawaida - ni jukumu la kila raia kujenga uelewa wa jinsi ya kua salama na kujenga tabia ya kufatilia taarifa zihusuyo usalama mitandao.
ReplyDeleteSwala la uhalifu mtandao linaonekana kutegemewa kushamiri zaidi nchi za afrika kutokana na uelewa wa jinsi ya kujikinga kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmjoa kua bado ni tatizo - Hivyo ni muhimu kila mmoja kuliangalia hili.
Takwimu zinatisha na nimeziandikia hapa (http://ykileo.blogspot.com/2014/06/dola-bil-400-zapotea-kutokana-na.html) - Na hatuna budi kujijengea utayari hasa pakizingatiwa matukio mengi ya hivi karibuni.
Mwisho - Kuelimisha jamii inakua rahisi kama ushirikiano kutoka katika vyombo vya habari na maeneo mengine ya sanaa yata shiriki - Wenzetu walioendelea wamekua wakifanikiwa kwenye hili kutokana na maweneo yote muhimu kujua nafasi zao kutoa mchango na kufanyia kazi ( Mfano Hollywood)