Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Ahmet Davitoglu, (mwenye miwani) akikata utepe kwenye hafla ya Uzinduzi wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha MWANA, kilichopo enero Vingunguti jijini, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kituo hicho kimejengwa na Shirika la Misaada ya Kimataifa, Turkish International Cooperation Development Agency (TIKA) na kimegharimu Dola za Marekani, 165,000. Wengine katika picha ni Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davitoglu, wakiwa wameandamana na maofisa wengine wa Uturuki wakiwemo wake zao.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Ahmet Davitoglu (wa pili kushoto) akiwapigia makofi vijana wa kituo hicho waliokuwa wakitoa burudani ya kuimba na kucheza.
Uturuki, imeahidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania ukiwemo usaidizi katika sekta za Ulinzi, Afya na
huduma za jamii ikiwemo kusadia kuwahudumia watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino, na Kujenga
Vituo vya Yatima ikiwemo kuvihudumia.
Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Ahmet Davitoglu, alipofanya ziara katika
meli 4 za kijeshi za Uturuki, zilizotia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam na baadae kuzindua kituo cha
kulelea watoto yatima cha MWANA, Vingunguti jiji Dar es Salaam jana mchana.
Bw. Davitoglu, amesema uhusiano kati ya Uturuki na Tanzania utazidi kuimarishwa kwa Uturuki
kuisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii ikiwemo kuboresha huduma za Afya
Elimu na kusaidia watu wenye Ulemavu wa ngozi Albino.
Amesema Waturuki wanawaona Watanzania kama ndugu zao na ndio maana wanawasaidia, ambapo
watajenga kituo cha kutunzia watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino, ambapo kinatarajiwa kugharimu
dola za Marekani zaidi ya milioni 10, na kinatarajiwa kutunza watu zaidi ya 500 ambao pia watapatiwa
elimu ya ujasiliamali na kuwezesha kujitegemea.
Akizungumzia ufadhili wa vituo vya yatima katika uzinduzi wa Kituo cha yatima cha Mwana kilichopo
Vingunguti jijini Dar es Salaam, Bwana Davitoglu amesema Uturuki, kupitia Shirika Lake la Misaada ya
Kimataifa, Turkish International Cooperation Development Agency (TIKA) utajenga vituo kadhaa vya
yatima na kusaidia kuviendesha.
Akishukuru kwa msaada huo. Mkuu wa kituo hicho, Mohamed Wage, ameishukuru serikali ya Uturuki na
shirika hilo la TIKA, Kkuwa ufadhili huo, ni msaada mkubwa sana kwa kituo chake, kinachotunza watoto
yatima zaidi ya 120, wakiwemo watoto wenye ulemavu wa ngozi.
Akizungumzia ziara hiyo, Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davitoglu amesema lengo kuu la ziara hiyo ni
kukuza ushirikiano wa kijeshe baina ya jeshi la Uturuki na majeshi ya nchi 27 za pwani barani Afrika sio tuu
kuonyesha uwepo na uwezo wa kijeshi wa Jeshi la Wanamaji la Uturuki, bali pia kusaidia katika operetions
mbalimbali za kijeshi barani Afrika ukiwemo vita dhidi ya uharamia kwa Pwani ya Bahari ya Hindi.
Uturuki ni moja ya mataifa makubwa yenye nguvu kubwa za kijeshi la la majini, tangu enzi za utawala
wa kale wa dola la Ottoman ambapo walitawala bandari nyingi barani Afrika ikiwemo miji ya Kilwa,
Sofala, na Lamu kwatika Pwani ya Bahari ya Hindi.
Hapo jana jioni, bendi za Jeshi la Tanzania na Uturuki, zimefanya onyesho la pamoja ambapo kivutio
kikubwa ni pale Waturuki walipoimba nyimbo kwa lugha ya Kiswahili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...