BONDIA wa zamani wa ngumi za kulipwa
nchini, Iraq Hudu 'Kimbuga' (49) amefariki
dunia, baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Dada wa Marehemu Tiba Takadiri, alisema kuwa
Hudu amefariki jana majira ya saa 11 ya alfajiri
kwenye hospitali ya Hindu Mandal, alikokuwa
amelazwa.
Takadiri, alimesema kuwa mazishi ya Hudu
yatafanyika leo kwenye makaburi ya Kisutu, Dar
es Salaam.
Alisema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa
na tatizo la ini na figo kutofanya kazi, ambapo
vilimsumbua kwa muda mchache kabla ya
kufariki kwake.
"Marehemu alilazwa hospitali Hindu Mandal
siku tatu zilizopita, ambapo majuzi jioni
alizidiwa
na jana asubuhi kukutwa na umauti", alisema Dada Tiba.
Hudu amezaliwa mwaka 1965 Ujiji Kigoma, na
kupata elimu ya msingi mkoani humo na
baadae kuja Dar es Salaam ambapo alimaliza
shule ya Sekondari na baadae kuanza shughuli
za ngumi katika miaka ya 1990 mpaka miaka ya
2000 alipoacha.
Marehemu ameacha watoto watatu, ambao ni
Daniel alikuwa akitarajia kufunga ndoa Juni 20,
wakati mtoto mwingine Msawila ambaye ni
mwanafunzi wa darasa la sita.
Maandalizi ya msiba yanaendelea nyumbani
kwa marehemu Buguruni Lozana Dar es Salaam
ambapo kesho saa 7, atazikwa Kisutu.
Marehemu Hudu aliwahi kutamba akiwa na
mabondia kina Joseph Marwa, Stanley Mabesi,
na baadae wakaja mambondi wengine Rashid
Matumla na Maneno Osward 'Mtambo wa
Gongo'.
Mwenyezi mungu aiweke roho ya marehumu amina
Marehemu Iraq Hudu (kulia) enzi za uhai wake akiwa na mwanae Daniel Hudu siku kijana wake huyu alipokula nondozzz yake katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Novemba mwaka jana.
Daniel na familia yake walikuwa katika maandalizi ya harusi aliyopanga kuifanya Juni 20, mwaka huu. Globu ya Jamii inatoa pole kwa wafiwa kwa msiba huu mzito.
Iraq Hudu alikuwa mmoja wa wadau wetu wa karibu sana na Michuzi Blog ambapo yeye marehemu na nduguye Sensei Rumadha Fundi aliyeko Marekani alikuwa mshauri mkubwa wa kazi zetu.
Mola Ipunzishe kwa amani
roho ya marehemu peponi - Amin
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...