Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ukiongozwa na Jamal Malinzi Juni 21 mwaka huu mjini Dodoma umekutana na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Said Mtanda (Mbunge wa Mchunga).

Katika kikao hicho TFF ilielezea mikakati yake ya maendeleo ya mpira wa miguu pamoja na maandalizi ya timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Msumbiji.

TFF iliiahidi Kamati ya Bunge kuwa itaendelea kuwa inafanya shughuli zake kwa karibu na Serikali na kamati hiyo ya Bunge.

Katika kikao hicho, ujumbe wa benki ya CRDB ukiongozwa na Meneja wa Electronic Banking, Bw. Mangire Kibanda ulihudhuria ili kutoa ufafanuzi juu ya mradi wa kuuza tiketi za elektroniki, mradi ambao maandalizi yanaendelea vizuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...