Mmoja wa
wadau wa shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi akitoa maoni yake kuhusu
namna ya kuboresha rasimu ya Sera ya Petroli. Wanaofuatia ni baadhi ya wadau
kutoka Kampuni mbalimbali zinazofanya
shughuli hizo nchini.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (katikati)
akifuatilia kwa karibu wadau wakitoa maoni wakati wa warsha ya wadau wanaoshughulika na shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi na
mafuta ili kupata maoni yao yatakayosaidia kuboresha Rasimu ya Sera ya
Petroli. Wa Kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Umeme
Mhandisi Innocent Luoga, wa pili kulia ni Kamishna Msaidizi Nishati, anayeshughulikia Petroli
Mhandisi Stanley Marisa na wa kwanza kulia ni Mjiolojia Mwandamizi Wizara ya Nishati na Madini, Adam Zuberi.
Washiriki katika warsha ya wadau wanaoshughulika na shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi na mafuta ili kupata maoni yao yatakayosaidia kuboresha Rasimu ya Sera ya Petroli
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava ( Wa nne kutoka
kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa
shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi na mafuta mara baada ya kufungua warsha hiyo. Picha na Asteria Muhozya
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...