Ndugu wanachama, Wadau na wandishi wote wa Habari, 
 Kuna ujumbe unaozunguka miongoni mwetu, kwa wandishi wa habari wasiokuwa wanachama na kwa wadau wetu ukieleza kwamba Mbeya Press Club (MBPC) imeandaa safari ya wanachama wake kutembelea nchi Jirani ya Malawi. 
Ujumbe huu unawataja baadhi ya wanachama wa MBPC kuwa ndio waratibu wa Safari hiyo, huku ukiwataka wanachama na wadau kuchangia safari hiyo fedha kiasi cha shilingi 200,000 (Laki mbili) kwa kila mwanachama na mwandishi wa habari yeyote asiyekuwa mwanachama wa MBPC. 
Kwa niaba ya uongozi wa MBPC napenda kuwataarifu Wanachama wa MBPC, Wandishi wa Habari wasiokuwa wanachama na wadau wetu kuwa mpango huo hauna utashi wala Baraka za MBPC, hivyo kwa yeyote Atakayejihusisha na mpango huo atambue kuwa atafanya hivyo kwa dhamana yake mwenyewe na sio ya MBPC. 
MBPC inawataka na kuwaonya wanachama na watu wasiokuwa wanachama walio nyuma ya mpango huo kuacha mara moja kutumia jina la MBPC katika kuratibu mambo yao la sivyo hatua kali dhidi yao zitachukuliwa. 
Uongozi wa MBPC unawataka watu hao kama wanaona mpango huo una kila sababu ya kutumia jina la MBPC wafike ofisini na kufuata taratibu zote ili kupata Baraka za MBPC. 
Mwisho naomba kuwaasa wanachama wa MBPC kutojihusisha wala kuupapatikia mpango huo kwani kuna dalili kuwa mwisho wake sio mzuri.
 Nawatakieni kila la Heri 
Emmanuel Lengwa – KATIBU MBPC. 
Asante.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...