Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini jana wakitokea Ethiopia Kocha wa Timu ya Riadha aliyeambatana na wachezaji 8 Bw. Shaban Hiiti alisema kuwa ana imani kubwa na wachezaji wake walioteuliwa katika Timu ya Taifa kuwa watailetea heshima Taifa kwa kuwa mazoezi waliyoyapata wakiwa nchini Ethiopia yamewajengea uwezo mkubwa.
Alisema  kuwa walipokuwa nchi Ethiopia kwa mazoezi wamejifunza mbinu mbalimbali kutokana na kuwa na program za kuwajengea uwezo wachezaji wake na wako tayari kwa mashindano ya  Jumuiya ya Madola 
“Nimatumaini yangu wachezaji hawa walioteuliwa kujiunga na wenzao waliokuwa mazoezini katika nchini zingine ambapo wanamichezo wetu walienda kwa ajili ya mazoezi wataliletea Taifa letu heshima kubwa kwani wamepikwa wakapikika”. Alisema Kocha huyo. 
Aidha kocha huyo amesema kuwa uwepo mazingira mazuri na vifaa bora vya mazoezi kumechangia kwa kiasi kikubwa kuinua ubora wa wanariadha hao ambao wamefanya mazoezi kwa takribani miezi miwili nchini Ethiopia. 
Kwa upande wake mmoja wa wanariadha ambaye amebahatika kuitwa kwenye kikosi kitakachoshiriki mashindano hayo Bw. Alphonce Felix amesema kuwa anajisikia faraja kuwa miongoni mwa wanamichezo watakao iwakilisha nchi katika mashindano ya Olympic kupitia mchezo wa riadha. 
Alphonce amesema kuwa atatumia ujuzi alioupata nchini Ethiopia walipokuwa wameweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.
 Jumla ya wanariadha 9 na kocha wao waliweka kambi nchini Ethiopia ikiwa ni jitihada zinazofanywa na Serikali za kukuza na kuendeleza Sekta ya Michezo nchini kupitia mpango wa Diplomasia ya Michezo, ambapo wanamichezo mbalimbali wameweka kambi ambao wanamichezo wengine waliweka kambi katika nchi za Uturuki, China na New Zealand
 Kocha wa wachezaji wa Riadha waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya  Jumuiya ya Madola  yanayotarajia kufanyika kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya wanamichezo hao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
 Kocha wa wachezaji wa Riadha waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajia kufanyika kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya wadau wa mchezo wa Riadha waliojitokeza kuwapokea wachezaji wa mchezo huo mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
: Kocha wa wachezaji wa Riadha waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya  Jumuiya ya Madola  yanayotarajia kufanyika kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya wanamichezo hao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana. Picha na Frank Shija - MAELEZO

Kwa habari zaidi ya michezo hiyo BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2014

    Jiangalieni msipate malaria au dengue hapa DSM maana ni joto na siyo baridi kama Ethiopia au Arusha, hivyo mkiweza mkapige kambi Arusha au Tukuyu kuepuka magojwa ya maeneo yenye joto Tanzania.

    Mdau
    Medali Lazima

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2014

    Malaria na degue kibao DSM mmetoka Addis Ababa kwenye baridi bora mgefikia Arusha au Tukuyu maana tunataka medali, wiki hizi mbili au tatu hapa DSM zinatosha kupata magonjwa ya maeneo ya joto Tanzania.

    Mdau
    Tukuyu, Mbeya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...