Sehemu ya waombaji zaidi ya 10,000 wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi, Idara ya Uhamiaji wakifanya usaili wa awali wa kuandika ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ajili ya kujaza nafasi 70 za kazi ambazo zinahitajika katika Idara hiyo. Usaili huo uliongozwa na Maafisa Utumishi wa wizara hiyo, umefanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo ambapo baada ya wiki moja waliofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho.
Afisa Utumishi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Penina Isamuyo akigawa makaratasi ya mitihani kwa waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi, Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya kufanya usaili wa awali wa kuandika. Zaidi ya waombaji 10,000 walifanya usaili huo Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo ambapo baada ya wiki moja watakaofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho.
Afisa Utumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwanamridu Jumaa (aliyevaa kiraia) na askari Magereza wakiwa wamebeba maboksi yenye makaratasi ya mitihani ya usaili iliyofanywa na zaidi ya waombaji 10,000 Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo. Baada ya wiki moja waombaji waliofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akisimamia usahihishaji wa mitihani ya usaili ya waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji inayosahihishwa na Maafisa Utumishi wa wizara na askari Magereza. Zaidi ya waombaji 10,000 wamefanya usaili wa awali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kugombea nafasi 70 zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akisimamia usahihishaji wa mitihani ya usaili ya waombaji wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji inayosahihishwa na Maafisa Utumishi wa wizara na askari Magereza. Zaidi ya waombaji 10,000 wamefanya usaili wa awali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kugombea nafasi 70 zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lubert Fransis (kulia) na Mwanamridu Jumaa wakipanga maboksi kwa ajili ya kuhifadhia makaratasi ya mitihani ya usaili. Zaidi ya waombaji 10,000 walifanya usaili wa awali Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo ambapo baada ya wiki moja waliofaulu vizuri wataitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
This is one big joke... nafasi 70 ... watu wamejaza uwanja wa taifa... hakiyamungu tutafika kweli??? Natumani walao watawaonea huruma haki itendeke isijeikawa yaleyaleee kuwa watu tayari wanajulikana hii danganya toto - waste people's time and give them fake hopes!!! MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE!!
ReplyDeleteHoi shughuli Ni pevu...! Nafasi 70 waliomba Ni 10000.
ReplyDeleteKweli ukosefu wa ajira Ni bomu linalokaribia kuripuka
Taabu mtupu kuona vijana 10000 wanawania nafasi 70, hii inaonyesha kwa jinsi wasomi wanavyokaa mitaani baada ya kumaliza masomo yao! Mungu iombee Tanzania yetu iondokane tatizo hilo ambalo linaletwa na wanasiasa.
ReplyDeleteLahaula.......siamini macho yangu...ni kweli umati huu upo ktk usaili???nilipoona jukwaa mawazo yangu yote yakagonga Brazil ila nilipoanza kua makini ndio nakutana na habari kamili. Kiukweli hizi ndizo habari haswa mnazopaswa kuzipa kipa umbele ili hata nasi wa mbali kuweza pata picha halisi na si kutuletea wingi wa ziara za kichama japo wenda mkawa mnalazimika kufanya hivyo ila sidhani kama zina tija kama uhalisia ndio huu wa usahili wa nafasi 70 kwa waombaji 20,000!!!
ReplyDeleteDu! Kweli hali ya ajiri bongo ni ngumu. Nafasi 70 waombaji 10,000.
ReplyDeleteHummmm! Hii ndo short list ama vp wenzetu???!!!!
ReplyDeletefor me sdhani sio kila aliyekuja kufanya uasili hao hana ajira kuna wengi tu wana ajiara zao. Mi naona tatizo hapo ni la kiufundi zaidi , haswa katiaka propoer recruitment . There was a bigh weakness in setting up job sepcification and communicating it to the proper audience. Also, there was a big weakness in shortlisting candidates. The criteria used were so broad in such a way that they couldn't objectively filter candidate who closely match with specifications . by the way specification were already poor. This has caused a lot of cost to the recruiter and candidates. I doubt about integrity and professionalism of those responsible for this exercise . Mimi naona hii ni fiasco na kuna watt ni lazima wawajibije kea hili
ReplyDeleteWasomi tumekuwa wengi sana. Ajira zipo kwa watu wachache. Haya tunaambiwa tujiajiri. Tutajiajiri bila kuwa na pesa ya mtaji? Mungu atusaidie kwa kweli.
DeleteHao bara tu Znz hawamo ingekuwaje
ReplyDeleteIdadi halisi niliyosikia ni 10500 kwenye radio asubuhi kwa hiyo 10500-70= 10430 wanarudi mitaani
ReplyDeleteHapa naona kuna tatizo la kiufundi katika recruitment.Questions to ask: 1;Was there a need to shortlist such a BIG number of candidates for a small number of vacancies?
ReplyDelete2.Who is carrying these recruitment cost burdens?Of course the govt.Tutafika kweli?
3.Will integrity be adhered to with such a big number of interviewees being tested through a written test?
Au ndo mambo yamebadilika kwamba wote wanaoomba wanaitwa kusailiwa!
We still have a long way to reach.