Na. Ally Mataula
Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wametakiwa kuzingatia maadili wanapokuwa wanatimiza majukumu yao ya kila siku. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Ikulu Bw. Peter Ilomo wakati akifungua Mkutano wa kumi na mbili wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma uliofanyika Jijini Mbeya tarehe 28 Mei, 2014. 
Bw. Ilomo alisema kuwa jukumu kubwa la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni kusimamia Maadili ya Viongozi wa Umma, hivyo basi ni muhimu kwa watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuzingatia maadili mema. 
Bw. Ilomo aliendelea kufafanua kuwa huwezi kuwa mwangalizi wa maadili ya wengine wakati wewe mwenyewe huna maadili mema. 
 “Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na watumishi wengine wa umma katika nyanja ya Uadilifu. Pamoja na changamoto nyingi mnazokabiliana nazo katika kazi zenu za kusimamia Maadili, ninawaomba sana Msikubali kuyumba au kuyumbishwa. 
Muendelee kufuata misingi ya Utawala Bora na Maadili mema katika utendaji kazi kwa kuepukana na Rushwa na kushinda vishawishi vya Rushwa na tamaa nyinginezo” alisisitiza Bw. Ilomo. 
Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua Mkutano huo Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda alisema kuwa ili kusogeza huduma karibu na wananchi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilianzisha Ofisi za Kanda ambapo mpaka sasa kuna Ofisi za Kanda saba katika Mikoa ya Arusha, Mbeya, Tabora, Mtwara, Mwanza, Kibaha- Pwani na Dodoma. 
Mhe. Kagana alutumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa Kuweza kuridhia kuongeza wigo wa Viongozi wanaowajibika na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ambapo Maafisa Ugavi Wakuu wa Wizara, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Serikali za Mitaa, pamoja na Viongozi mbalimbali waliopo Serikalini. 
 Pia , Mhe Kaganda aliomba Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iwezeshwe kwa kuongezewa bajeti yao pamoja na idadi ya watumishi. 
Mikutano ya Mabaraza ya Wafanyakazi ni utekelezaji wa Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 1970 wenye lengo la kuwashirikisha Wafanyakazi katika kubuni, kushauri na kupendekeza namna bora ya uendeshaji na utendaji kazi.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Ikulu Bw. Peter Ilomo katikati akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda wa pili kutoka kulia pamoja na Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi  wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma uliofanyika jijini Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...