Semi-Trela likiwa limebeba kontena likiwa limeanguka baada ya kulielemea  kwa uzito na kulivunja daraja la chuma katika barabara ya Banana-Kinyerezi maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam leo. Haikuweza kufahamika mara moja lilikuwa limebeba mzigo gani na kama dereva alikuwa anajua daraja hilo ni kwa magari yenye uzito wa wastani  wa tani 7 tu au ni kiburi tu.  Hakika Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli  na jeshi lake wana kazi ya ziada kuhakikisha uzembe kama huu hautokei na haujirudii. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2014

    Tanzania naililia Tanzania yangu kila siku balaa utafikiri ndio kwanza tumetoka kwenye mahandaki.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2014

    Aina hii ya ajari na zenye kufanana nazo hutokea Tanzania pekee.......kila uchao tunashuhudia mambo kama haya wakati mwengine yakigharimu maisha ya wasio na hatia.....ni huzuni kubwa sana....kulizunguka tatizo kana kwamba halina ufumbuzi.....

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 20, 2014

    solution ya kuwatia adabu hawa malori

    yawe na insurance kubwa inayoweza lipa huu uharibifu na madhara ya hizi ajali

    gari likikutwa halina insurance mmiliki afungwe jela pamoja na faini

    kwa haya heshima itarudi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 20, 2014

    Ni sawa na msemo ''Gari Haijai Abiria'' na huyu dereva wa lori alikuwa na mawazo hayo hayo akiongeza '' Ujanja Kuwahi'' na mwisho tunasema '' Ni Kazi ya Mungu'' daraja kuvunjika.

    Mdau
    Christos Papachristou
    Diaspora

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 20, 2014

    Mpiga picha amesahau kupiga kile kibao cha tani 7 kilichopo mita chache kabla ya daraja. Lori lilikuwa limejaza matofali kwenye hilo container la futi 40, piga mahesabu ujue lilikuwa na tani ngapi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 20, 2014

    Si magufuli alithalilishwa kwa kuweka faini kwa magari yanayozidisha uzito? Mtafuteni waziri mkuu aseme ni kitu gani kimesababishwa daraja kuvunjika.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 20, 2014

    This is beyond STUPIDITY, let the driver and his company pay for rebuilding this bridge. Utterly disgusting way of squandering (kutapakanya) Tanzanians monies, hii ni pesa ya mkulima na mfanyakazi, mijitu mingine haisikii mpaka UICHAPE FIMBO, aaarrrrggggghhhhh!!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 20, 2014

    Mwenye Lori na mwenye mzigo watiwe ndani na Magufuli ahakikishe daraja linajengwa kwa gharama za hao wamiliki. Huu ni uzembe usiovumilika hutokea sana hata pale daraja la Mlalakuwa magari ya zaidi tani 7 hupita na Askari wapo lakini hatua hazichukuliwi. Mheshimiwa Magufuli uwe mkali sana kuhusu hili jambo.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 20, 2014

    HILI GARI LITAUIFISHWE NA DEREVA ANYONGWE, KWANI GARAMA YA KUJENGA DARAJA HILI NI SAWA NA SHULE ZA MSINGI 20 AU DISPENSARY ZA VIJIJINI 25 HII NI HASARA KUBWA SNA KWA UCHUMI WA NCHI MASKINI KAMA HII

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 20, 2014

    Naona sasa upole tuweke kando,kwa nini sipewi ushauri mkuu kwa mh Magufuli? Hapa ni mwenye gari kulipa gharama zote za matengenezo ya daraja bila kuchelewa. Kinyume chake ni kutaifisha gari na mzigo. Wenye magari wakishaonja joto ya jiwe watajua jinsi ya kuadabisha madereva wao. Kila siku tunapiga mark time hatusongi mbele shauri ya ujinga wa wachache kama huyu dereva!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 20, 2014

    MSimlaumu mwenye kubeba mizigo mizito ni WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA juzi tu ameruhusu magari yaliyojasza mpaka pomoni kupita kwenye barabara na watu wamepigia kele sana hili nashangaa ni waziri mkuu wa aina gani huyu? kauli zake nyingi ni utata tu

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 20, 2014

    HUKUMU YA PAPO KWA PAPO ZA RISASI ZINAHUSU

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 20, 2014

    kweli akili ya muafrika ni kama andazi ,chai maharage. ndiyo maana wazungu wanatuona kama akili zetu ni sawa na nyami kwani ubongo wetu bado kukomaa-
    Muafri´ka oyee

    Kuma mbegese

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 20, 2014

    nilikuwepo eneo la tukio na hiyo njia mchepuko tuliyopita ilitufikisha home saa 4, kwakweli hatufiki, Magufuli hawezi kuwa na macho nane, palepale wangeweka mechanism to ensure no lorry crosses the temporary bridge sasa ndio hiyo ilikuwa njia mchepuko yetu kwa wakazi wa kimara na kibamba ukichukulia maanani kuwa morogoro road imefungwa kupisha matengenezo, heri tutafute vyumba upanga

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 20, 2014

    Mengi yatasemwa, lakini ifike mahali madereva wapimwe akili kwanza kabla hawajaendesha magari, sababu kwa mtu tu wa kawaida huwezi kutoa uamuzi wa kupitisha container kama hili kwenye daraja dogo la chuma kama hilo wakati alama zipo. Pia kuwe na utaratibu wawepo polisi jamii kwenye hizi njia, nasema hivyo sababu barabara za kutokea mandela kwenda tabata ni nyembamba na uwezo ni mdogo wa kupitisha Semi trailer, malori makubwa na matenki. Tumeshuhudia mara nyingi magari hayo yanaanguka na kuleta madhara, lakini cha kushangaza hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wazembe hawa. Pia wakati mvua zilipokuwa zinanyesha zilileta mafuriko maeneo mbalimbali hapa Dar ikiwepo kona ya kuelekea CCM kwenda Kimanga barabara ilimegwa, ikabidi bila kutoka saa kumi alfajiri nyumbani, utachelewa kazini sababu foleni ilikuwa inaanzia Kimanga, lakini bila aibu malori yaliendeelea kupita na matenki ya mafuta, sasa huu upole uishe jamani, sasa hivi sisi wenyewe wananchi tuwe walinzi sababu ndio tunaopata matatizo kila siku, bajeti zenyewe za serikali ndio hizo. Inabidi tusimame kidete kukomesha wapuuzi kama huyo dereva aliyevunja daraja. Sbb ameshaleta athari kubwa sana kwa wakazi wa maeneo mengi. Ushauri wangu ni kwamba mzigo huu sio tu apewe Waziri Magufuli, sisi wenyewe wananchi tuwe na msimamo kuhusu hawa watu wasiokuwa na masikio, sbb sasa hivi adha ya foleni imeongezeka mara dufu toka jana kuelekea Tabata-Segerea-Kinyerezi na maeneo mengineyo.

    Mwisho mmiliki ajenge daraja letu, akileta ubishi jera, hapo hakuna msamahaaaaaaaa!!!!!

    Tumechoka jamaniii!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 21, 2014

    Mdau umesema kweli akili ya mwafrica ni kama andazi hivi kweli ata kwa ufikilio tu angepita kwenye hilo daraja. na tani zote hizo, hmmm kama wanavyosema wenzetu watu weusi ubongo mdogo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...