Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akioneshwa vipande vya madini aina ya Tanzanite ,katika mgodi wa mchimbaji mzawa wa madini ya Tanzanite Bi.Suzie Didas Kennedy.Katibu Mkuu wa CCM alitembelea migodi ya wachimbaji wadogo wa Mererani na kuzungumza nao juu ya changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua. Pichani kati aneshuhudia ni Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh.Christopher Ole Sendeka.
 Moja ya jiwe lenye madini kabla ya kufanyiwa mchakato. 
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia namna wachimbaji wadogo wanavyotumia mashine kubebea mchanga kutoka kwenye mgodi wa mchimbaji mzawa wa madini ya Tanzanite Bi.Suzie Didas Kennedy.Katibu Mkuu wa CCM alitembelea migodi ya wachimbaji wadogo wa Mererani na kuzungumza nao juu ya changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mererani wilaya ya Simanjiro ambao wengi ni wachimbaj wa wadogo wadogo wa madini kwenye mkutano wake wa mwisho baada ya kumaliza ziara ya siku 26 ambapo alitembelea mikoa mitatu ya Tabora, Singida na Manyara.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mererani ambao aliwaambia vyama vya Upinzania ni sawa na Jogoo kwani hata awike vipi hawezi fungua mlango na kwa sababu vyama hivyo havipo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi basi vinaelekea kufa kwani havina sera mpya za kujinadi kwa wananchi.
 Jengo la Kituo cha Afya cha Mama na Mtoto Endiamtu,Mererani Simanjiro,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alikwenda kukagua na kujionea ujenzi wake ulipofikia
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akitoka kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Mama na Matoto cha Endiamtu,Mererani wilayani Simanjiro.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa tanki la maji litakaloweza kuhudumia watu 25,000 na kutoa  lita 36,000 kwa saa linalojengwa Naisinyai Mererani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2014

    Hotuba ya Bw.Kinana inapatikana?Tunahitaji kufahamu alichoongea(Kinana) tupate msimamo wake kuhusu sakata la juzi Bungeni DODOMA kati Prof.Muhongo na Bw.Sendeka au litajadiliwa na vikao 'vya ndani' vya CHAMA?

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...